Home Azam FC AZAM FC ‘WAIGONGA KMC YA HITIMANA’ KWA MBINDE…NDEMLA AITAKATISHA MTIBWA MANUNGU…

AZAM FC ‘WAIGONGA KMC YA HITIMANA’ KWA MBINDE…NDEMLA AITAKATISHA MTIBWA MANUNGU…


Baada ya ukame wa muda mrefu, hatimaye Timu ya Azam FC ‘Waoka Mikate wa Dar’ wameibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Wakusanya Ushuru wa Kinondoni ‘KMC’ jioni ya jana Jumamosi, Mei 7, 2022.

Mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC umepigwa katika Dimba la Chamazi ambapo mabao yote mawili ya Azam yakifungwa na Rodgers Kola dakika ya 2 na dakika ya 36 huku bao la KMC likifungwa na Miraji Athumani dakika 48 ya mchezo huo.

Azam sasa wamepanda nafasi moja kutoka nafasi ya nne ya Ligi mpaka nafasi ya tatu wakiwa na jumla ya pointi 32 nyuma ya Yanga wanaoongoza ligi wakiwa na pointi 56 na Simba Sc wa pili wakiwa na pointi 43.

Michezo mingine iliyopigwa mapema leo ni ule kati ya Geita Gold na Kagera Sugar ambapo Geita katika Dimba lao la Nakumbu wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0, bao pekee lililofungwa na mshambuliaji mzawa George Mpole dakika 5 ya kumfanya afikishe mabao 12 ya Ligi sawa na Fiston Mayele aliyekuwa akipngoza kwa mabao hayo hayo 12.

Aidha, wakata miwa wa Mtibwa Sugar wakiwa nyumbani katika Dimba la Manungu kule Turiani wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City, bao la Mtibwa limefungwa na Said Ndemla dakika ya 16.

SOMA NA HII  WAKATI MECHI YA SIMBA vs YANGA IKIPANGWA KUCHEZWA CCM KIRUMBA...GEITA GOLD KUISAIDIA SIMBA....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here