Home Habari za michezo BAADA YA KUISHIA JUKWAANI MSIMU ULIOPITA…MAKAMBO AVUNJA UKIMYA KUHUSU YANGA MPYA…ATOA MSIMAMO...

BAADA YA KUISHIA JUKWAANI MSIMU ULIOPITA…MAKAMBO AVUNJA UKIMYA KUHUSU YANGA MPYA…ATOA MSIMAMO WAKE…


Mshambuliaji wa timu ya Yanga, Heritier Makambo raia wa Congo DR amesema kikosi chao cha msimu huu utakaoanza hivi karibuni ni kikali kuliko kikosi cha msimu uliopita hivyo wana kila sababu ya kufanya vizuri katika ligi ya ndani na mashindano ya Kimataifa.

Makambo amesema hayo wakati akifanyiwa mahojiano kuhusu maandalizi ya msimu mpya huku akiwataja nyota wapya waliosajiliwa wameongeza chachu ya kufanya vizuri zaidi kwa kikosi hicho.

“Maandalizi ni magumu kidogo lakini yanaendelea vizuri, lazima tuyafuatilie program za mwalimu kwa sababu itatusaidia kwa msimu mzima.

“Msimu uliopita ulikuwa mgumu lakini tunashukuru Mungu tumemaliza kwa furaha. Nafahamu Wanayanga wanatarajia msimu ujao Makambo ajaze zaidi (afunge), ndio maana tunajaribu kufanya maandalizi ya kuwapa furaha zaidi.

“Naona timu itakuwa zaidi ya ilivyokuwa mwaka jana, nawapongeza viongozi wetu kwa usajili ambao wameufanya, wachezaji wapya wameongeza chachu na sisi tuliokuwepo tunafanya kweli. Kwa hiyo kwa wachezaji ili upate nafasi lazima ufanye vizuri kwenye mazoezi. Tunaamini kwenye ligi na kimataifa tutafanya vizuri sana,” amesema Makambo.

SOMA NA HII  RASMI....KILIO CHA YANGA KUHUSU WAAMUZI CHASIKIKA...TFF WACHUKUA MAAMUZI HAYA ...