Home Burudani BWANAEEH…KUMBE ISHU YA DIAMOND KUHAMIA YANGA UKWELI WAKE UKO HIVI…

BWANAEEH…KUMBE ISHU YA DIAMOND KUHAMIA YANGA UKWELI WAKE UKO HIVI…

Habari za Yanga

Staa wa Bongo Fleva, Nsibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ametangaza rasmi kuacha kuishabikia Simba SC na sasa anaishabikia Yanga SC.

Diamond ametangaza jambo hilo usiku wa kuamkia leo Januari 19, 2023 kwenye hafla ya kuzaliwa ya Haji Manara iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City.

“Mimi sikuwa mtu wa mpira, nilijiunga kuishabikia Simba kwa sababu ya Manara sasa kwa kuwa amehamia Yanga basi na mimi ni Yanga,” alisema Diamond.

Diamond alisema yeye kwenye maisha yake anapenda kushabikia timu inayoshinda na ndio maana msimu uliopita Yanga ilichukua ubingwa na msimu huu vilevile watachukua.

“We si umeona tulichukua ubigwa na mwaka huu tunachukua kama unavyoona kwenye msimamo tunaongoza ligi,” alisema Diamond.

Manara alikuwa msemaji wa Simba SC kisha akaachana na Wekundu hao na kuchukua nafasi ya usemaji Yanga SC lakini hata hivyo baadaye alikumbana na rungu la kufungiwa miaka miwili na TFF.

SOMA NA HII  BAADA YA KUSHUSHIWA MASHINE YA KAZI...GAMONDI AANZA UPYAA YANGA...