Home Habari za michezo KOCHA UGANDA “YANGA WATAWAPIGA RIVERS…AMEZUNGUMZA HAYA

KOCHA UGANDA “YANGA WATAWAPIGA RIVERS…AMEZUNGUMZA HAYA

KOCHA UGANDA

Yanga inajiandaa kumalizana na Simba kwenye Kariakoo Derby,
kisha kusafiri kwenda Nigeria kuvaana na Rivers United katika mechi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, huku kocha wa zamani wa timu hiyo anayoiona kwa sasa timu ya taifa ya Uganda The Cranes, Milutin Sredojevic ‘Micho’ ameipa nafasi kubwa ya kuvuka hatua hiyo kwenye nusu fainali ya michuano hiyo.

Kocha huyo aliyeinoa Yanga mwaka 2007, alisema kwa uzoefu alionao kwa timu za Afrika na anaona nafasi kubwa uwezekanao wa kufuzu kwenda nusu fainali kwa asilimia 75 kutokana na mabadiliko makubwa waliyoyafanya kikosini.

Micho alisema Yanga kuwa na Fiston Mayele aliye kinara wa mabao Ligi Kuu akiwa na 16 na mwenye muendelezo mzuri wa kufunga anaamini ataendelea kuibeba timu hiyo sambamba na nyota wengine ambao wameivusha Yanga tangu ilipokuwa Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Nimeifundisha Yanga, kuna mabadiliko makubwa ya kiuchezaji na hata aina ya wachezaji, nisemeni mechi na Rivers innatabirika kwani sasa hivi Yanga ina kiungo mzuri kama Khalid Aucho ambae anaichezea timu ya taifa ya Uganda, Mayele na wengine wanaoweza kuipigania na kuivusha,” alisema.

Yanga itacheza na Rivers kwenye mechi ya mkondo wa kwanza itakayochezwa Aprili 23 ugenini kabla ya kurudiana Aprili 30 jijini Dar es Salaam na timu itakayofuzu hapo itakutana na mshindi wa mechi kati ya Pyramids ya Misri na Marumo Gallants ya Afrika Kusini.

SOMA NA HII  YACOUBA AMPA JEURI KAZE