Home Habari za michezo JEZI N0 20 YAPIGWA STOP SIMBA…..ISHU YA MKUDE YATAJWA…

JEZI N0 20 YAPIGWA STOP SIMBA…..ISHU YA MKUDE YATAJWA…

Habari za Simba

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema katika kumuenzi legendari Jonas Mkude, jezi namba ishirini aliyokuwa akiivaa haitatumika msimu ujao.

Ahmed ameyasema hayo kupitia Simba APP ambapo pamoja na mambo mbalimbali aliyoyatolea ufafanuzi, alizungumzia suala la Mkude na madai ya kwamba klabu haijamuaga kwa heshima.

“Mkude amekaa miaka zaidi ya 13, ametuvumilia kwenye nyakati ngumu nasi pia tumemvumilia. Aametoka timu ya vijana hadi kuweka alama kubwa kwenye timu ya wakubwa, hatuwezi kumuacha hivi hivi. Tutamuaga kwa heshima zote,” alisema Amhed.

Meneja huyo wa habari alisema, Simba ndio muasisi wa kuwaaga wachezaji vizuri hivyo wataendeleza utaratibu huo kwa Mkude na hata wachezaji wengine waliotoa mchango katika klabu.

“Hata hizi thank you unazoziona sisi ndio tulizianzisha, wengine ilikuwa unasikia tu kwenye magazeti, yawaacha nyota kadhaa. Sisi ndio tulifanya hivi kwa kina Kagere, Tadeo Lwanga, Pascal Wawa na wengine.

“Tuliwalipia nauli wakaja kwenye Simba Day na wakaagwa kwa heshima zote. Kina Pascal walizunguka uwanjani na kupewa heshima na hata hela na mashabiki,” alisema Ahmed.

Ahmed alimaliza kwa kusema, jezi ya namba ishirini ya Mkude, haitavaliwa na mtu Simba mpaka pale atakapopatikana kijana na makocha wakajiridhisha ana uwezo kama wa Mkude basi watamkabidhi jezi hiyo.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUZIDI KUFANYA MAAJABU YANGA..GSM WAMWEKA 'KITI MOTO' MAYELE...MWENYEWE AANIKA A-Z...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here