Home Habari za michezo SIMBA ATAMBA UGENINI, AWANYOOSHA WALIMA MIWA MANUNGU

SIMBA ATAMBA UGENINI, AWANYOOSHA WALIMA MIWA MANUNGU

simba

IKIWA Uwanja wa Manungu, Morogoro katika safu za milima ya Uluguru, Mtibwa Sugar imeyeyusha pointi tatu.

Ubao umesoma Mtibwa Sugar 2-4 Simba ukiwa ni mchezo wa ufunguzi Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24.

Katika mchezo wa Agosti 17 Uwanja wa Manungu, Mtibwa Sugar walikuwa imara kwenye mashambulizi ya kushtukiza pamoja na kujilinda kwa tahadhari huku wakikosa kutumia nafasi ambazo walizipata.

Mabao ya Simba yamefungwa na Jean Baleke dakika ya tano, Willy Onana dakika ya 9, Fabrice Ngoma dakika ya 44 na Clatous Chama dakika ya 80.

Mwamba aliyewatungua Simba dakika 45 za mwanzo ni Matheo Anthony ilikuwa dakika ya 20 na 22 kwa Mtibwa Sugar amemtungua Ally Salim mabao yote mawili.

SOMA NA HII  KUMEKUCHA FEI TOTO ATAKA KULIANZISHA TENA AZAM, ADAI HANA FURAHA