Home Habari za Simba Leo BAADA YA KUACHWA MIQUISSONE AFUNGUKA KILA KITU…KUHUSU SIMBA

BAADA YA KUACHWA MIQUISSONE AFUNGUKA KILA KITU…KUHUSU SIMBA

Habari za Simba

ALIYEKUWA mchezaji wa Simba na Winga wa Kimataifa wa Msumbiji Luis Jose Miquissone amefunguka kila kitu kuhusu yeye kutemwa mitaa ya Msimbazi, huku akiweka wazi kwamba Simba itabaki kuwa timu kubwa.

Jioni ya Juni 19, saa12 kasoro kasoro, Taarifa za kushtua kwa mashabiki na wapenzi wa soka Tanzania zilisambaa mitandaoni kote, zikieleza kwamba Uongozi wa Simba umeshindwa kumuongeza mkataba mwingine mchezaji huyo.

Kupitia video fupi aliyoirekodi, Miquissone alifunguka mambo mengi ndani ya klabu hiyo, huku akiwashukuru mashabiki zake na mashabiki wa timu hiyo.

“Hii ni taarifa yangu, nafikiri mitandao ya kijamii imekwiaha weka wazi kila kitu, ndio nathibitisha hilo, sitokuwa sehemu ya Simba”

Ni ukweli Simba itabaki kuwa timu yangu, Simba ni klabu kubwa, huo ndio mpira muda mwingine unatakiwa kuachana na timu moja ili kwenda sehemu nyingine, cha muhimu ni heshima kutoka kwa watu.” Luis Miquissone

Mchezaji huyo alirejeshwa katika klabu hiyo baada ya kusajiliwa na Al ahly, kisha kutokuwa na kiwango kizuri, badae miamba hiyo ilimtoa kwa mkopo na Simba ilimrejesha akiwa kamaliza mkopo wake na Al ahly.

Lakini tangu arudi Simba hajawahi kuwa na yale makali yake ya zamani, kasi ilipungua kutokana na kuwa na uzito mkubwa, chenga na uwezo wa kupiga mbali vyote vilikosekana, hali hiyo ilimpelekea mchezaji huyo kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu, huku baadhi ya mechi akitokea kama mchezaji wa akiba.

Miquissone ndiye alikuwa mchezaji ghali zaidi kwenye ligi kuu ya NBC, alikuwa anavuta mshahara wa zaidi ya Tsh Milion 47, huku mkataba wake ukiwa na kipengele cha bonasi ya dola 200 akifunga goli, dola 100 kama akitoa pasi ya goli.

Lakini pia katika mkataba huo, kulikuwa na kipengele cha kuvunjiana mkataba bila malipo kwa Simba endapo mchezaji huyo hatokuwa na kiwango kizuri kwa mwaka mzima, na ndicho kilichomuondoa Simba.

KWAHERI LUIS MIQUISSONE, OBRIGADO JOSEE

SOMA NA HII  NGOMA BADO MBICHI TFF...SIMBA VS COASTAL UNION...MJUMBE MMOJA ATIMULIWA KWENYE KIKAO