Home Habari za Simba Leo LUIS MIQUISSONE APEWA THANK YOU SIMBA…

LUIS MIQUISSONE APEWA THANK YOU SIMBA…

HABARI ZA SIMBA

UONGOZI wa Simba umefikia hatua ya kutangaza kuachana na nyota wake Luis Miquissone baada ya kushindwa kukubaliana suala la kumuongeza Mkataba.

Miquissone alikuwa na mkataba wa miaka 2 Simba ambao aliusaini mwaka jana 2023, lakini baada ya kushindwa kuonesha makali kwenye msimu huu Simba imeamua kumuacha.

Katika mkataba wake alioutumikia kwa mwaka mmoja tu, ulikuwa na kipngele cha kuwaruhusu kumvunjia mkataba endapo atashindwa kuonesha kiwango kizuri.

Miquissone ni moja ya wachezaji wachche wa kigeni waliokuwa wanalipwa vizuri kwa klabu ya Simba, na ndiye alikuwa anaongoza kwa kulipwa mshahara mkubwa zaidi kuliko mchezaji yeyoye yule.

Mshahara wa Miquissone kwa mwezi ulikuwa unafika Tsh Milion 47, huku akiwa na bonasi za kila mechi, bonasi ya goli au ya kutoa pasi ya goli.

Baada ya kuachwa na Simba na kujiunga na miambaya Afrika, Al Ahly Miquissone hakuonesha makali, na klabu hiyo ilimtoa kwa mkopo, baadae akakaa karibia msimu mzima bila kucheza mechi za mashindano.

Simba ilimrudisha mchezaji uyo, huku akiwa na uzito mkubwa, alipewa programu maalum ya kupunguza uzito wake lakini hakuwa na kiwango kizuri. Kuanzia kwa kocha Robertinho, Benchika na hata kwa Mgunda.

Klabu ya Simba bado inaendelea na safisha safisha kwenye kikosi chake kabla ya kuanza utambulisha sajili  mpya, ambazo tayari wameshamaliza kazi ya kuwapa mikataba.

SOMA NA HII  MO DEWJI APANGA SAFU MPYA YA MASHINDANO SIMBA