Home Habari za Simba Leo SAFISHA INAENDELEA SIMBA…CHILUNDA AKUTANA NA FAGIO LA CHUMA

SAFISHA INAENDELEA SIMBA…CHILUNDA AKUTANA NA FAGIO LA CHUMA

HABARI ZA SIMBA

KATIKA kuendelea kufanya maboresho ya kikosi cha timu hiyo, uongozi wa Simba umetangaza kuachana na mshambuliaji wake mzawa  Shaban Chilunda baada ya mkataba wake kufikia tamati.

Imeelezwa kuwa  Waziri Junior yupo kwenye rada za kutakiwa na Simba ambaye ipo katika mchakato wa kuongeza mshambuliaji mzawq baada ya kuachana na Chilunda na John Bocco ambaye amestaafu soka.

Waziri ameanza kujadiliwa na wekundu hao kwenda kuitumikia klabu hiyo kwa nafasi ya mshambuliaji mzawq baada ya kuonyesha kiwango kizuri alipokuwa KMC FC msimu uliopita akimaliza Ligi Kuu Bara akifunga mabao 11.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba,  Ahmed Ally amesema  Chilunda amemaliza mkataba wake wa mwaka  mmoja na hatakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kaa msimu wa 2024/2.

Amesema mchezaji kijana mwenye kiwango kizuri, alijiunga na Simba kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye nafasi ya kuongezewa endapo wangeridhishwa na kiwango chake.

“Kipindi cha dirisha la mwezi Januari Chilunda alicheza kwa mkopo KMC hadi mwisho wa msimu lakini sasa hayupo kwenye mipango ya timu kuelekea msimu ujao.

Simba inaamini katika uwezo wa nyota huyo na inamtarajia kufanya makubwa katika timu ambayo itamsajili, hayo ni sehemu ya maboresho ya kikosi kwa msimu ujao,” amesema Ahmed.

Amesema baada ya kukamilika kwa mchakato wa kuwapa ‘Thank you ‘, wachezaji hao, watakuja kuweka wazi waliongezewa mikataba na mwisho watawatambulisha siraha zao mpya zilizosajiliwa kuanza kazi msimu ujao.

“Wanasimba watulie viongozi wanafanya usajili mkubwa kulingana na mahitaji ya timu yetu pamoja na mapendekezo ya benchi la ufundi kujenga Simba imara na bora,” amesema Ahmed.

SOMA NA HII  SIMBA KUPELEKA TUZO YAO YA CAF KWA HAYATI MAGUFULI....MPANGO MZIMA UKO HIVI..