Home Habari za Yanga Leo HATMA YA MASTAA 3 YANGA KUJULIKANA…YUMO SKUDU

HATMA YA MASTAA 3 YANGA KUJULIKANA…YUMO SKUDU

Habari za Yanga leo

HATMA ya mastaa watatu wa kigeni Yanga, kujulikana Julai Mosi mwaka huu wakati uongozi wa timu hiyo kutangaza rasmi siku hiyo ni maalum ya kuwapa ‘Thank you “ wachezaji hawataoendelea nao kwa msimu wa 2024/25.

Wachezaji ambao wanadaiwa kutokuwa sehemu ya timu kwa msimu ujao ni Mahlatsi Makudubela (Skudu), Joyce Lomalisa na Augustine Okrah.

Kwa mujibu ofisa habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema kuanzia Julai Mosi mwaka huu, timu hiyo itaanza kuwatangaza wachezaji watakaoachana nao na kuongezewa mkataba.

Ameeleza sababu ya kuchelwa kutangaza wachezaji wanaowacha kutokana na mipango yao waliyojiwekea pamoja na kuchelewa kwa kupewa barua nyota wapya wamewasijili kutoka klabu zao.

“Matarajio yetu ifikiapo Julai Mosi, mwaka huu tunatangaza wanaoacha na wanaongezewa mikataba, kuna wachezaji tayari tumeshamalizana nao lakini bado hawajapewa barua kutoka klabu walizotoka na kumaluza mikataba yao.

Tumefanya usajili mkubwa sana kwa sababu malengo yetu ni kuhakikisha tunaendelea kufanya vizuri ndani na michuano ya Kimataifa kucheza fainali ya Afrika, inatulazimu kusajili wachezaji bora,” amesema Kamwe.

Kuhusu suala la deni na kupelekea kufungiwa kusajili na Shirikisho la Kimataifa la mpira wa miguu (FIFA ), Kamwe amesema hakuna kesi yoyote ambayo inawahusu klabu hiyo kwa sababu ameshamalizana na wachezaji walikuwa wakiidai Yanga.

“Wachezaji hao ni Mamadou Doumbia na Lazorous Kambole wote tumeshamalizana nao Juni 14, mwaka huu siku moja kabla dirisha kubwa la usajili kufungiliwa ambao ilikuwa Juni 15, jana tumepokea Email kutoka Fifa ikitoa siku tano kukamilisha usajili wa Kambole kwenye system,” amesema Kamwe.

Ameongeza kuwa suala la Okra litawekwa wazi muda utakapifika kuendelea kusalia ndani ya kikosi cha timu baada ya mapendekezo na mipango ya kocha Gamondi (Miguel).

Okrah ambaye klabu Bechem United (Ghana) imeishtaki Fifa klabu ya Yanga kushundwa kulipa hesemu ua ada ya uhamisho wa nyota huyo.

Imeelezwa kuwa ada ya uhamisho ni dola za kimarekani 120,000 (Million 313,800,000 za Tanzania), Yanga imeripotiwa kulipa dola 20,000 (Mill 52,300,00) kwa qjili ya kupata ITC ya mchezaji hali hiyo bado wanadaiwa dola 100,000 sawa na Mill. 261,500,00

SOMA NA HII  MANARA AWAITA ORLANDO PIRATES...'"NJOONI WANAUME...WANANCHI WEZENU TUPO....