Home Habari za Simba Leo BREAKING NEWS…CHAMA AMALIZA MKATABA SIMBA…MO DEWJI AMUITA DUBAI KIMYA KIMYA.

BREAKING NEWS…CHAMA AMALIZA MKATABA SIMBA…MO DEWJI AMUITA DUBAI KIMYA KIMYA.

Habari za Simba leo

MOJA Kati ya mchezaji aliyegonga vichwa vya habari na habari yake kuwa ya moto sana kwa takribani wiki ya pili sasa Clatous Chama, mkataba wake na Simba ni rasmi umeisha leo Juni 30.

Lakini kuna habari nyingi za yeye kuhitajika na Yanga ambao miaka mingi wamekuwa wakimtamani, huku upande wa Simba ukiwa unaendelea kumshawishi abaki ili asaini mkataba mpya angalau wa mwaka mmoja tu.

Mashabiki na wanachama wa Simba wamegawanyika kwenye sakata hili, wapo wanaotaka Chama Asepe tu na wengine wanaona abaki klabuni, huku wengine wakiwa hawajulikaniwapo upande gani, ni 50/50.

Moja kati ya shabiki mkubwa wa Simba aliyefuungiwa hivi karibuni, ameandika ujumbe huu akisema kwamba Chama atabaki kuwa mali ya wanasimba. Huku meneja habari wa Simba Ahmed Ally nae akigongelea msumari kwa kusema kwamba “Chama kama Viogozi wanamuhitaji watambakiza”

“Maamuzi ya kumuachia aondoke yalikuwa yamefikiwa tayari na sehemu kubwa ya uongozi ilikuwa imeridhia aondoke ndani ya timu hiyo mara baada ya mkataba wake kufika ukingoni.” Dr Mohammed- Shabiki na Mwanachama wa Simba tawi la VIP B.

“Ghafla upepo ukabadilika mara baada ya Bilionea kijana ambaye ndio mwenyekiti wa bodi Ya Wakurugenzi ya Simba SC MOHAMEDI DEWJI Kubadili maamuzi na kuamua kumbakisha ndani ya timu hiyo mara baada ya kumuita Dubai na kumalizana naye kiutu uzima imeisha hiyo.

“Clatous Chama ataendelea kuwepo ndani ya kikosi cha Simba msimu ujao kuanzia sasa hii kesi tumeifunga rasmi this case is closed.

“Huu umekuwa ni msimu wa 4 mfululizo sasa Chama anasajiliwa Yanga lakini anacheza Simba na safari hii wameikosa pia saini yake tena kwa mara nyingine labda wajaribu tena mwakani.

“Wana Simba bakini humu hii ndio taarifa sahihi na ya ukweli kuhusu CHAMA hakuna taarifa nyingine tena itakayokuwa tofauti na hii tunachokisubiria tu ni taarifa rasmi sasa kutoka page ya Simba na app ya Simba kupost taarifa hii ili maisha mengine yaendelee.” Aliandika Dokta Mohammed Shabiki wa Simba.

SOMA NA HII  BAADA YA KUTINGA ROBO FAINAL KIBABE...MBRAZILI SIMBA AAPA KUIVIMBIA YANGA...APELEKA FAILI 'KWA MABOSI KAZI'...