Home Habari za Simba Leo MAGORI AZIDI KUFANYA UMAFIA ZAMBIA…AWAFICHA NYOTA WAWILI WA ZECO UTD

MAGORI AZIDI KUFANYA UMAFIA ZAMBIA…AWAFICHA NYOTA WAWILI WA ZECO UTD

Habari z simba

MABOSI wa Simba hawataki mchezo kabisa, wanachokifanya kwa sasa ni kuhakiisha wachezaji wanaowasjili wanasifa za kuitwa timu zao za Taifa, pia huko Zambia masta mmoja anafanya zake fujo ya usajili balaa.

Inaelezwa kwamba Crescentius Magori ameshaimsainisha winga kiberenge Joshua Mutale kutoka Power Dynamos ya huko lakini akawaita chemba wachezaji wawili, akianza na kiungo mkanajo Kelvin Kapumbu kisha baadaye beki wa kati Tandi Mwape

Zesco Utd ya Zambia, ilikuwa inapambana kuwaongezea mikataba Tandi Mwape na Kapumbu, ili kutengeneza ukuta imara kwa ajili ya msimu ujao itakaposhiriki mashindano sawa na Simba ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Upande wa Zesco wanaumiza kichwa kutokana na kwamba mastaa hao wawili wa timu ya taifa ya Zambia, wamekuwa wasumbufu ghafla kuendelea na mazungumzo wote wakitajwa kutiwa kiburi na Simba kupitia mazungumzo na Magori.

Akitolewa ufafanuz juu ya sakata hilo ambalo linaonekana kuingiliwa na Magori, Bosi wa Zeco Utd alisema;

“Kapumbu amekuwa hataki kupokea simu, tunataka kumuongezea mkataba, huku pia Tandi (Mwape) naye tulikuwa tunakwenda naye vizuri lakini amekuwa hajibu tena simu zetu na wote wawili walionekana na kiongozi wa Simba alipokuja hapa,” alisema bosi wa juu wa Zesco Utd ambao ni Mabingwa wa zamani wa Soka nchini humo.

Mnyama SIMBA YUPO Mawindoni katika kuhakikisha wanapata wachezaji wazuri, watakaoisaidia timu  hiyo kurejesha makali yake yaliyopotea kwa misimu mitatu iliyopita.

SOMA NA HII  TANZANIA YATIKISA AFRIKA...SOKA LA BONGO LAPATA HESHIMA CAF