Home Habari za Simba Leo WAWILI WAONGEZWA…KAMATI YA USAJILI SIMBA

WAWILI WAONGEZWA…KAMATI YA USAJILI SIMBA

HABARI ZA SIMBA LEO

NI MWENDO wa Kimya kimya tu baadae kila kitu kitakuwa sawa, Simba naona wamechagua kufanya mambo yao kwa siri, hususani mabadiliko ndani ya Uongozi na Sajili za wachezaji ili kurudi kwenye ile hadhi yao ya Simba kwa Mkapa Hatoki Mtu.

Baada ya kukaa na kugundua kuwa kilichoikwamisha Simba kwa kipindi cha misimu mitatu ni aina ya usajili ambao ilikuwa inafanya

Sasa maamuzi na hatua stahiki zimeanza kuchukuliwa, unakumbuka siku zilizopita Soka La Bongo tuliripoti mabadiliko ya Kiungozi ndani ya klabu hiyo, ambapo Magori na Sued Nkwabi kurudishwa kamati ya usajili.

Hatimaye tena kuna sura mbili za kazi zimerudishwa, ili kuongeza nguvu kwenye kamati ya usajili wa Simba, majina hayo ni Mulamu Nghambi, Kassim Dewji.

Viongozi hawa awali kipindi Simba inasumbua sana hawa watu walikuwa sehemu ya kamati hiyo iliyopewa jina la Kamati ya roho mbaya na kimafia, ikiongozwa na Marehemu Hans Pope.

Kinachoendelea Simba SC ni suala la mabadiliko ya kiungozi, amapo MO Dewji amethibitisha kurudi moja kwa moja ndani ya Simba baada ya kujiweka mbali na mambo ya kufatilia na kusajili.

Pia Barbara Gonzalez amerudishwa ndni ya klabu hiyo, ili kuongeza nguvu zaidi kwenye utendaji haswa, upande wa kutengeneza mvuto wa timu, kuvutia masoko na wadhamini wengine, pia kufanya sajili na kurejesha makali ya Mnyama yaliyopotea.

SOMA NA HII  "KUNA WATU WAMEWEKEZA PESA WANA...MICHAMBO,MASIMANGO NA MINUNO"...ALLY KAMWE