Home Habari za Simba Leo FADLLU DAVIDS ANATAKA KUWEKA REKODI CAF

FADLLU DAVIDS ANATAKA KUWEKA REKODI CAF

HABARI ZA SIMBA-FADLU

KOCHA Mkuu wa Simba, Fadlu Davids, amewaambia wanachama na mashabiki wa timu hiyo kuwa wawe na subira kidogo, kwani kikosi chake kinaelekea kwenye ubora anaouhitaji, na ana uhakika itakuwa ni tishio zaidi si hapa nchini tu bali Afrika.

Fadlu alitoa kauli hiyo juzi, baada ya kumalizika kwa mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya timu hiyo na Tabora Uited, ikishinda mabao 3-0, Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.

Kocha huyo alisema bado anaendelea na kazi yake ya kukiimarisha kikosi hicho, lakini akiridhika na jinsi walivyocheza na kupata ushindi huo.

“Timu inaanza kuimarika, siku hadi siku inaelekea kwenye ubora ninaotarajia, mashabiki wa Simba wawe na subira kwa sababu bado tunaendelea kukiweka kikosi kwenye hali nzuri, na kukifanya kiwe bora zaidi na tishio.

“Bado tuna shughuli ya kufanya, ukiangalia katika mechi hii ilikuwa tuiue mapema tu kipindi cha kwanza na kipindi cha pili tucheze bila presha kwa kuudhibiti na kuumiliki mchezo, lakini haikuwa hivyo.

“tukalazimika kusaka mabao ya kuumaliza mchezo kipindi cha pili, lakini nimeridhika, ila nimehuzunika kuumia kwa Mutale (Joshua), kidogo kidogo tunakwenda,” alisema Fadlu ambaye ndiyo msimu wake wa kwanza kuifundisha timu hiyo akitokea, Raja Casablanca ya Morocco.

Yalikuwa ni mabao ya beki wa kati, Fondoh Che Malone, Valentine Mashaka na Awesu Awesu, yaliyofanya Simba kupata ushindi wa mabao 3-0, yaliyoipeleka kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu.

SOMA NA HII  MAYANGA ATENGENEZEWA UFALME MITBWA SUGAR...KOCHA ATHIBITISHA