Home Habari za Simba Leo MUKWALA NA FREDY WALIVYOZINGUA SIMBA

MUKWALA NA FREDY WALIVYOZINGUA SIMBA

Habari za simba-mukwala

KLABU ya Simba imesajili washambuliaji watatu hadi sasa, mzawa Valentino Mashaka na Steven Mukwala raia wa Uganda, wameingia kikosini hapo kuongeza nguvu eneo la ushambuliaji kwa kushirikiana na Freddy Michael aliyekuwapo tangu dirisha dogo msimu uliopita.

Baada ya Simba kucheza mechi mbili za Ngao ya Jamii na moja ya Simba Day, washambuliaji hao wakashindwa kumshawishi Fadlu kuendelea kuwaamini, hivyo akaagiza asajiliwe mshambuliaji mwingine. Kitendo hicho ni wazi washambuliaji hao wamemzingua Fadlu kwani mwanzo aliamini wanatosha lakini imekuwa tofauti.

Kuongeza nguvu eneo la ushambuliaji, Simba imemalizana na Leonel Ateba raia wa Cameroon, mchezaji ambaye Fadlu anaamini hatamuangusha.

β€œUjio wa Mshambuliaji mpya utakuwa chachu ya ushindani na kuendelea kumuimarisha Karabaka ambaye naamini atakuja kuwa Mshambuliaji tishio hapo baadae kutokana na umri wake na amekuwa akiimarika siku hadi siku,” alisema Fadlu.

SOMA NA HII  KOCHA MORROCO AFICHUA MBINU ZA WYDAD...AWAPA MBINU HIZI SIMBA