Home Habari za Simba Leo SASA IMEISHAA…SIMBA NA YANGA WAANZA KUTAMBIANA KUELEKEA AGOSTI 8.

SASA IMEISHAA…SIMBA NA YANGA WAANZA KUTAMBIANA KUELEKEA AGOSTI 8.

Habari za Simba na Yanga

UKISIKIA funga kazi, basi ilikuwa jana wakati Yanga ilipohitimisha Kilele cha Wiki ya Mwananchi, saa 24 tu tangu Simba kufanya tamasha la Simba Day na kutambilisha mashine mpya za msimu wa 2024-2025m, huku mashabiki wa timu hiyo baada ya kuona vikosi vyote kutamba wakisema ‘Tukutane Nane Nane’.

Simba na Yanga zinatarajiwa kuvaana Alhamisi hii kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa katika pambano la nusu fainali ya Ngao ya Jamii, ikiwa Dabi ya Kariakoo ya kwanza msimu huu, huku kila upande ukiwa umeimarisha vikosi ilivyonavyo ambapo wikiendi hii zilikiwasha katika matamasha yao maarufu.

Katika mechi ya msimu uliopita, Simba iliitambia Yanga katika Ngao ya Jamii kwa kuifunga penalti 3-1 baada ya muda wa kawaida kumalizika kwa suluhu, lakini ilipigwa nje ndani katika Ligi Kuu, ikianza kwa kuchapwa 5-1 kabla ya kufungwa tena 2-1 na kujikuta ikimaliza nafasi ya tatu nyuma ya Yanga na Azam FC.

Hivyo, mashabiki wa klabu hiyo wanaona ni muda muafaka wa kukutana na wenzao Alhamisi kumaliza ubishi, kwani kila moja ikiamini ina kikosi bora kitakachofunika Kwa Mkapa kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Bara Agosti 16. Washindi wa mechi hiyo ya Simba na Yanga ataumana na yule wa mechi kati ya Azam na Coastal Union zitakazocheza pia Agosti 8 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Unguja.

Sasa wakati mashabiki wa klabu hizo wakianza kuchimbana biti mapema kabla ya timu hizo kukutana Agosti 8, kilichofanywa jana na Yanga Kwa Mkapa ni kama kujibu mapigo kwa watani, wao baada ya Wananchi kuwahi mapema na kupata burudani ya kuhitimisha Kilele cha Wiki ya Mwananchi.

SOMA NA HII  KABLA YA HATA MSIMU KUANZA RASMI....SIMBA WAMEWEKA REKODI HII YA KIBABE MAPEMA TU YANI...