Home Habari za Simba Leo SIMBA IMESAJILI VIZURI…SHIDA IKO HAPA

SIMBA IMESAJILI VIZURI…SHIDA IKO HAPA

HABARI ZA SIMBA-fREDDY

SIMBA SC kwa miaka karibu minne iliyopita walikuwa bora sana kwenye eneo la mwisho kwa kutazama hata idadi ya magoli waliyifunga kwa msimu husika, washabuliaji wengi na hata viungo wao wa juu ambao walipita kwa wakati huo walichangia namba kubwa sana ya magoli tofauti na miaka ya hivi karibuni ilivyo ndani ya Ligi Kuu na mashindano makubwa.

Binafsi naona eneo la mwisho lina presha kubwa sana na mashabiki wengi wa Simba hata wengine ndio wanatazama kama eneo ambalo nguvu yake kwa sasa inapaswa kuwa kubwa sana! Baada ya Meddie Kagere na John Raphael Bocco kutozalisha magoli mengi na baadae kuondoka imepelekea eneo la mwisho kukosa nguvu kama ilivyokuwa awali

Wachezaji wengi waliokuja katika eneo hilo imekuwa ngumu kufanya vizuri, nadhani inatokana na presha kubwa pia ambayo wameikuta ya wachezaji wengi ambao wameondoka katika eneo hilo kuwa na namba nzuri ambazo zimetengeneza mazingira magumu kwao! Kwa sasa Timu inahitaji utulivu tu kwa watu ambao wapo ili kutoa namba nzuri katika eneo hilo

Kwa sasa Fadlu David’s anahitaji kutengeneza njia nzuri ya washabuliaji wake ili kupata magoli mengi kutoka kwao lakini pia kuunda mfumo mzuri wa Timu kuzalisha magoli kutoka maeneo mbalimbali ya uwanja, yaani wale Kelvin Kijili, Shomari Kapombe, Valentine Nouma, Mohamed Hussein na wengineo kwenye eneo la nyuma watengeneze uwiano mzuri wa kuipa Timu magoli

NO DOUBT! Simba wamefanya usajili mzuri wa vijana wengi ambao naona wanahitaji mud tu ili kupata Timu nzuri ambayo itatoa ushindani mkubwa kuanzia mashindano ya ndani na nje, sio eneo la kiungo na ushambuliaji tu ndio linahitaji kuzalisha magoli bali hata eneo la nyuma lina nafasi kubwa ya kuboresha na kuzalisha magoli mengi.

Welcome to Tanzania, Lionel Ateba(25)

SOMA NA HII  DIARRA AFICHUA SIRI YA YANGA...AMTAJA AUCHO