Home Habari za Simba Leo SIMBA YAAMBULIA SARE NA AL HILAL…IBENGE AWAPA SOMO

SIMBA YAAMBULIA SARE NA AL HILAL…IBENGE AWAPA SOMO

HABARI ZA SIMBA

MCHEZO WA KIRAFIKI,  kati ya Simba SC na Al Hilal imemalizika kwa timu zote kutoshana nguvu ya bao 1-1.

Simba ilitangulia kufunga goli  kupitia kwa mshambuliaji wake mpya Leonel Ateba kipindi cha kwanza, lakini Al Hilal walifanya shambulizi la hatari na Serge Pokou aliisawazishia Al Hilal kwa kufunga moja ya goli gumu na zuri zaidi.

Baada ya mchezo huo, makocha wote wawili walizungumza kuhusu mchezo huo, lakini kubwa zaidi Florent Ibenge akiikubali Simba kuwa imempa mechi nzuri.

“Kipindi cha pili tulifanya mabadiliko tukacheza vizuri, lakini tukapata kadi nyekundi ila tuliweza kucheza kwenye aina yetu ya uchezaji na tukasawazisha goli”

“Simba ni timu kubwa imenipa changamoto nzuri, nafikiri hiki ni kipimo sahihi kwetu na hata kwa Simba” Amesema Falorent Ibenge

Kwa upande wa kocha wa Simba SC Fadlu Davids amesema kuwa Ateba amekuja kuongeza kitu kipya kwenye eneo lake la ushambuliaji.

“Ilikuwa ni nzuri kweli na tulichopanga kukipata tumefanikiwa, kwenye mashindano ya CAF timu zinakuwa na uwezo mkubwa, ninafuraha baada ya timu, unatakiwa kukutana na timu kama hizi”

“Sitaki kumuongelea mchezaji mmoja, kwa sababu Mashaka anatokea nje na anafunga, Mukwala ni hivyo pia kwahiyo hicho ndio tunachokitaka ushindani ndani ya uwanja”

“Namna ya goli lilivyofungwa huwezi kumlaumu kipa kwa sababu mpira umepigwa kwenye near post, ni ngumu sana kwa kipa kuruka maeneo kama yale” Koccha wa Simba Fadlu Davids.

SOMA NA HII  BAADA YA KUBANJULIWA 3-O JANA....JEMEDARI SAID KAIBUKA NA 'DONGO' HILI KWA YANGA...