Home Habari za Simba Leo SIMBA YATUMIA MAMILIONI USAJILI WA ATEBA…MWENYEWE AFUNGUKA

SIMBA YATUMIA MAMILIONI USAJILI WA ATEBA…MWENYEWE AFUNGUKA

HABARI ZA SIMBA-ATEBA

SIMBA imeshamshusha straika mpya Leonel Ateba baada ya kufikia makubaliano na USM Alger ya Algeria kwa ajili ya uhamisho wa raia huyo wa Cameroon ili kuimarisha safu ya ushambuliaji ya Wekundu iliyopo chini ya kocha Fadlu Davids aliyehitaji kuboreshewa zaidi eneo hilo.

Hata hivyo, wakati Simba inafanikisha uhamisho wa mshambuliaji huyo anayetazamiwa kuongeza nguvu eneo hilo, inaelezwa kuwa, haikuwa rahisi kumnasa kutokana na ugumu kiasi cha kocha na skauti wa timu hiyo kuumiza kichwa.

Inaelezwa kwamba Klabu ya Simba imetumia kiasi cha dola za Kimarekani 250000 sawa na Milioni 677 za Kitanzania, na huo unakuwa usajili mkubwa zaidi kwa klabu ya Simba msimu huu wa 2024/25.

Ateba Leonel Christian kama anavyofahamika huko nchini kwao Cameroon, akiwa USM Alger hakuwa na namba nzuri sana kutokana na kubadilishiwa majukumu yake.

Kiasili Ateba ni mshambuliaji wa kati na muda wote huwa anacheza kama namba 9,  lakini baada ya kufika Algeria kocha wa USM Alger alianza kumchezesha winga hii ikamfanya kuwa na asisti nyingi kuliko magoli.

Ujio wake utaenda kumpa msaada Steve Mukwala ambaye amekuwa akiteseka kwenye umaliziaji licha ya kuwa na mikimbio mizuri na kuwasumbua mabeki wa timu pinzani.

Ateba amechukua nafasi ya Kipa wa klabu ya Simba Ayoub Lakred ambaye,  alipata majeraha yatakayomfanya awe nje ya uwanja kwa muda mrefu kidogo.

SOMA NA HII  MDHAMINI WA SIMBA SIO KINYONGE MPANGA ZAMBIA