Home Habari za Simba Leo SIO KAWAIDA SIMBA KUKUBALI KUFUNGWA…WAPONGEZWA

SIO KAWAIDA SIMBA KUKUBALI KUFUNGWA…WAPONGEZWA

HABARI ZA SIMBA

Pongezi zielekezwe kwa Simba,wamesajili vizuri,wanaonyesha kuna pahala wanaelekea kuutafuta ubora walionao Yanga kwa takribani misimu mitatu mfungaji!

Yanga ilitengeneza upekee wake,kiasi cha kuwa ili uweze kuutambua ubra wa kikosi chako basi kipimo sahihi kimekuwa lazima kwanza ucheze na Yanga ndipo utakapojifanyia tathmini iwapo yaliyomo yamo ama lah!

Ubora wa Yanga umedhihirika hadi katika michezo ya kimataifa, hawabahatishi na hawaonyeshi kuchoka!

Nimefurahishwa kwa namna Simba walivyopokea matokeo kwa mikono miwili,na huo ndio uanamichezo!unakubali umezidiwa pahala,unakwenda kufanya tathmini ili urejee ukiwa mshindani na ushindi zaidi.

Sio jambo jepesi kuona wana Simba wanajipongeza tena baada ya kufungwa na mtani katika mechi ya tatu mfululizo, tafsiri yake wameamua kuishi katika uhalisia na wameanza kuamini katika mchakato na sio shortcut.

Wana Simba wao wenyewe wanaona wamepunguza gape baina yao na watani zao,ni matarajio yao kuwa ndani ya muda mfupi wataweza kufikia daraja la ubora walilopo Yanga.

Mtego ni huu,je kipimo cha ubora wa Yanga kitakua kimefikia ukomo?yani hapo tunapowaona hakuna uwezekano wakaisogeza gauge juu zaidi?watu wanajisahau kuwa Yanga nao bado kuna ubora wanautafuta ili wakashindane katika michuano ya Klabu bingwa barani Afrika.

Tafsiri yake Gamondi Muguel na vijana wake wanajua kuna kazi wanatakiwa waifanye!huenda tukaiona Yanga bora zaidi ya ile tuliyoiona !hivyo wapinzani wanapaswa kufanya kazi zaidi ili waweze kuipiku Yanga na si jambo la haraka sana,ni mchakato!

Ameandika David Kampista.

SOMA NA HII  SIMBA YACHAPWA FAINI NA BODI YA LIGI KISA HIKI HAPA