Home Habari za Simba Leo ELLIE MPANZU AONGEZA MZUKA SIMBA…ASAINI MITATU

ELLIE MPANZU AONGEZA MZUKA SIMBA…ASAINI MITATU

habari za simba-mpanzu

WINGA raia wa DR Congo Ellie Mpanzu rasmi amemalizana na Simba kwa kusaini dili la miaka mitatu kuitumikia timu hiyo ambayo inanolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

 

Ellie Mpanzu
Winga Mpya wa Simba SC, Ellie Mpanzu amesaini kuitumikia klabu hiyo miaka mitatu.

Ikumbukwe kwamba Septemba 22 Mpanzu alikuwa Uwanja wa Mkapa kushuhudia timu hiyo ikicheza mchezo wa raundi ya pili Kombe la Shirikisho kusaka mshindi wa kutinga hatua ya makundi na jambo hilo lilifanikiwa ubao uliposoma Simba 3-1 Al Ahli Tripoli ya Libya.

Simba walikuwa wanaiwinda saini ya Mpanzu ambapo walikuwa wanatajwa kumalizana naye kwenye dili la awali ila mambo yalibadilika nyota huyo akapata timu Ulaya mipango ilivyokwama huko akarejea DR Congo na kufufua mazungumzo yake na Simba hatimaye dili lake limekamilika.

Atakuwa ndani ya Simba kwa msimu wa 2024/25 dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa kwa kuwa hakuwa kwenye mpango wa mechi za awali msimu wa 2024/25 ambao una ushindani mkubwa.

SOMA NA HII  YANGA YAIJIBU SIMBA...MCHONGO UKO HIVI...SHUKA NAYO

1 COMMENT

  1. […] ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Simba kuichapa Al Ahli Tripoli mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam na kufuzu hatua […]

Comments are closed.