Home Habari za Simba Leo MPANZU AILILIA SIMBA…HATAKI TENA KUCHEZA AS VITA

MPANZU AILILIA SIMBA…HATAKI TENA KUCHEZA AS VITA

HABARI ZA SIMBA-MPANZU

IKO WAZI kwamba Winga Mcongo Ellie Mpanzu amefeli majaribio yake na KRC Genk,kwa sasa amerejea Kishansa kuangalia mustakabali wa maisha yake….ukweli ni kwamba Mpanzu hataki Tena kucheza Vita Club,ingawa bado wanajaribu kumshawishi.

Inaelezwa kuwa Simba wapo kwenye nafasi nzuri ya kuinasa saini ya Mpanzu kama wataamua kurudi tena, ni baada ya majaribio yao mawili kutofanikiwa kipindi cha dirisha kubwa la usajili.

Rais wa AS Vital Amadou Diaby analazimisha kumbakiza mchezaji huyo ambaye Uongozi wa klab hiyo, kabla ya kwenda Ubelgiji walikuwa wamemuahidi kumlipa mshahara mkubwa zaidi atakaolipwa na Simba, huku wakipanga kumpa Unahodha wa timu.

Kwa upande wa Simba bado wana nafasi ya kumpata mchezaji huyo kwani kwa upande wa Mpanzu anataka kutafuta changamoto mpya, na taari alishawaaga marafiki zake wa karibu, hivyo Simba wanapewa nafasi kubwa zaidi ya kuinasa saini ya winga huyo katika dirisha dogo la usajili mwezi wa kwanza.

SOMA NA HII  KUELEKEA MCHEZO WA PILI SAUZI....BARBARA AFUNGUKA 'KIBABE' NAMNA WATAKAVYOPITA 'KIMYA KIMYA'....