Home Habari za Simba Leo FADLU AMKINGIA KIFUA ATEBA…ANAJUA KUFUNGA

FADLU AMKINGIA KIFUA ATEBA…ANAJUA KUFUNGA

Habari za Simba- Ateba

Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amemkingia kifua mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Leonel Ateba 25, akisema anamwona akifika mbali msimu huu kwa jinsi anavyomsoma mazoezini kambini.

Akizungumza alisema, kwa ubora anaomuona nao mshambuliaji huyo na akiunganisha na viungo anaamini kuna kitu kizito kinajengwa msimu huu.

Alisema ni mshambuliaji wa tofauti sana hasa anapokuwa uwanjani unamwona kabisa kuwa ana njaa ya kupata ushindi na ndiyo maana alipopata nafasi aliitumia na kufunga.

“Ni mshambuliaji mzuri, kwani akiwa uwanjani unamuona anavyopambana, wakati bado akiwa mgeni kabisa, hii inaonyesha matumaini makubwa.

“Ninachotaka ni yeye kujiimarisha na kuungana na wachezaji wenzake hasa viungo ili waweze kuwa na ushirikiano mkubwa wa kutengeneza nafasi na kupata mabao.”

“Namuona Ateba akiwa na msimu mzuri kwa kufunga mabao ya kutosha kwani sasa vimebaki vitu vichache kama kuzoeana na wenzake ili aonyeshe makali zaidi,” alisema Fadlu Davids.

SOMA NA HII  SHABIKI SIMBA:- KWA MWENDO HUU YANGA BINGWA TENA...MZAMIRU NO 10 TANGU LINI...?