Home Habari za Simba Leo JEAN AHUOA ATUMA SALAM KWA WALIBYA

JEAN AHUOA ATUMA SALAM KWA WALIBYA

HABARI ZA SIMBA-AHOUA

KIUNGO mshambuliaji wa Simba anayeongoza kwa asisti kwa sasa katika Ligi Kuu Bara, Jean Charles Ahoua amerejea tena uwanjani akiwa fiti kwa asilimia 100 tayari kuivaa Al Ahli Tripoli ya Libya baada ya kuwa nje kwa majerahana kumpa kicheko Kocha Fadlu Davids aliyemtetea pia straika mpya, Lionel Ateba.

Ahoua alibainika kupata majeraha madogo ya misuli mara baada ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Fountain Gate na alifunga bao moja wakati Simba ikishinda 4-0 na kuanzishiwa programu maalumu na kocha wa viungo, Riedoh Berdien na kumfanya akose mechi ya kirafiki ya sare 1-1 kati ya timu hiyo na Al Hilal ya Sudan.

Baada ya ya kurudi uwanjani kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya JKT Tanzania, Ahoua alifunga bao la kwanza kwa mkwaju wa penati na kutoa ishara kwamba yuko fiti kuwavaa Al Ahli Tripoli siku ya Jumapili Septemba 15.

SOMA NA HII  INONGA AIPATIA SIMBA MIL 500...WAARABU WAMALIZA KILA KITU