Home Habari za Simba Leo SIMBA VS JKT TANZANIA KUCHEZWA BILA MASHABIKI

SIMBA VS JKT TANZANIA KUCHEZWA BILA MASHABIKI

Habari za Simba

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amesema mcheZo wa kirafiki kati ya Simba dhidi ya JKT Tanzania ambao utapigwa Jumamosi, Septemba 7 katika Uwanja wa KMC Complex hautahudhuriwa na mashabiki.

Awali ilielezwa kuwa mashabiki wangeruhusiwa lakini ametoa ufafanuzi kuwa kipindi hiki ambacho ni kalenda ya FIFA, inalazimu kucheza mechi ya ndani.

“Unajua sasa hivi ligi zimesimama kupisha kalenda ya FIFA, ratiba nyingine za michezo ya ndani zinaruhusiwa kuendelea lakini kwa utaratibu maalum”.

“Hivyo mchezo wetu dhidi ya JKT Tanzania utakuwa mchezo wa mazoezi (mechi ya ndani) ambayo mashabiki hawataruhusiwa kuingia”.

“Niwaambie mashabiki wa Simba hii ni kama mechi ya mazoezi tu, hakuna shabiki ataruhusiwa kuingja uwanjani,” alisema Ahmed Ally.

SOMA NA HII  AHMED ALLY ASHINDWA KUVUMILIA AITETEA SARE YA SIMBA,AFUNGUKA HAYA