Home Habari za Simba Leo SIMBA YAAMBULIA MEDALI…YANGA YASHINDWA KUTWAA NDOO

SIMBA YAAMBULIA MEDALI…YANGA YASHINDWA KUTWAA NDOO

Timu ya wanawake ya Simba SC, Simba Queens imefanikiwa kushinda nafasi ya tatu baada kuichakaza bila huruma magoli manne bila majibu timu ya CEASIAA katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa Ngao ya Jamii kwa timu za mpira wa miguu za wanawake.

Simba Queens ilitolewa na Yanga Princes hatua ya nusu fainali kwa mikwaju ya penati huku CEASIAA akitolewa na JKT Queens.

Baada ya mchezo huo, fainali inawakutanisha Yanga Princes na JKT Queens katika uwanja wa KMC hii leo.

SOMA NA HII  KISA 'MASHUSHU' WA WASAUZI.....SIMBA KUIKIMBIA KAMBI YAO YA MBWENI...WATAKA MATOKEO KAMA YA ASEC...