BEKI SIMBA AWAOMBA WATANZANIA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA
GADIEL Michael, beki wa Simba anayevaa jezi namba mbili amesema kuwa wakati huu ni muhimu kila mmoja akachukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.Beki huyo amesema kuwa kitu cha muhimu kwa kila mmoja ni afya hivyo ni muhimu kufuata kanuni na taratibu za Wizara ya afya ili kuwa salama."Ni janga kubwa ambalo lipo kwa taifa na dunia nzima kiujumla...
MLINDA MLANGO KAGERA SUGAR APATA MUDA WA KULEA BINTI WAKE
BENEDICT Tinoko, mlinda mlango wa Kagera Sugar amesema kuwa likizo ya lazima waliyopewa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona imempa nafasi ya kumwona binti yake.Binti huyo aliletwa duniani wakati kipa huyo akitimiza majukumu yake ndani ya Klabu ya Kagera Sugar.Nyota huyo amesema:-"Ukweli ni kwamba Corona imeharibu kwa kiasi kikubwa shughuli zetu lakini kwa upande wangu namshukuru Mungu kwani...
SIMBA QUEENS WAIKIMBIZA JKT QUEENS MAZIMA
KABLA ya shughuli za michezo kusimamishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona, kwa upande wa Ligi Kuu ya Wanawake Klabu ya Simba Queens ilikuwa inaongoza ligi.Ligi ya Wanawake inashirikisha timu nane ambapo 12 na bingwa mtetezi wa taji hilo ni JKT Queens.Klabu ya Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 29 baada ya kucheza mechi 11.Klabu ya...
LICHA YA KUWA NI NAHODHA HUYU NI MTAMBO WA KUTUPIA PIA NDANI YA KLABU YA SAHARE
KASSIM Shabani Haruna ni nahodha wa Sahare All Star FC inayoshiriki Ligi Daraa la Kwanza ametupia mabao manne na kutoa pasi nne akiwa amecheza mechi 12.Timu yao ipo nafasi ya 11 ikiwa ipo kundi B kibindoni ina pointi 19 baada ya kucheza mechi 18.Kinara wa kundi lao ni Gwambina FC iliyocheza mechi 18 kibindoni ina pointi 40.Kwa sasa Ligi Kuu...
MO AANZA KUFURU SIMBA NI NDANI YA CHAMPIONI JUMATATU
MUONEKANO wa Ukurasa wa mbele Gazeti la Championi Jumatatu lipo mtaani jipatie nakala yako nafasi ya kushinda ndinga mpya ni yako
HIKI NDICHO WANACHOKIKOSA WANA SIMBA KWA SASA
UONGOZI wa Simba umesema kuwa kikubwa ambacho wanakikosi kwa sasa ni zile furaha za mashabiki pamoja na uhondo wa mechi za Ligi Kuu Bara ambazo walikuwa wamezizoea.Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kukosekana kwa uhondo huo kunawapa mawazo kidogo ila kwa kuwa ni kwa ajili ya afya hakuna namna lazima iwe hivyo."Unajua tayari kikosi cha Simba kilikuwa...
HUYU NAYE KICHWANI ZIMO, UWANJANI ANA BALAA ANATAJWA KUTUA YANGA
PAUL Nonga, nahodha wa Lipuli, kichwani ana Stashahada ya Ulipuaji Miamba ambayo aliamua kujiongeza baada ya kumaliza kidato cha sita na aliipata kwenye Shirika la Elimu Mwanza.Ametupia mabao 11 na pasi nne za mabao na Lipuli ipo nafasi ya 13 baada ya kucheza mechi 29 na ina pointi 33 ikiwa imetupia mabao 35.Nonga anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi...
DODO YA ALIKIBA YAWEKA REKODI YA AJABU BONGO
MSANII wa Bongo Fleva, Alikiba, ameweka rekodi ya ngoma yake ya Dodo kukaa Youtube Trending kwa muda mrefu kuzidi ngoma yoyote iliyotoka mwaka huu.Hadi kufikia jana Ijumaa, Alikiba alifikisha siku ya tisa kukaa Youtube Trending kwa Tanzania tangu kutoka kwa ngoma hiyo Aprili 8, mwaka huu.Ngoma kama Gere ya Tanasha na Diamond, Jeje ya Diamond nazo zilikaa kwa zaidi...
MSHAMBULIAJI HUYU AMEPIGA KITABU, UWANJANI ANATUPIA KAMA KAWAIDA
WAZIR Jr, mshambuliaji huyu anakipiga Mbao FC. Kichwani ana Degree ya IT ana tuzo pia ya mchezaji bora wa Mwezi Novemba ambapo aliipata baada ya kutupia mabao manne wakati timu yake ya Mbao ilipocheza mechi nne.Amehusika kwenye mabao tisa kati ya 19 yaliyofungwa na Mbao ambapo amefunga saba na kutoa pasi mbili za mabao.Timu yake ipo nafasi ya 19...
KAGAME AENDELEA KUMSHIKILIA KAGERE..!!
SERIKALI ya Rwanda, imeongeza muda kwa wananchi wake kukaa ndani na mipaka kufungwa hadi Aprili 30, mwaka huu kutokana na janga la virusi vya corona, hivyo kuondoa matumaini ya mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere, kurejea nchini Tanzania kwa sasa.Awali baada ya ugonjwa wa Corona kuingia nchini humo, Rais wa nchi hiyo, Paul Kagame, alitoa agizo la wananchi wake kukaa...