BIASHARA UNITED : TUMEJIPANGA KULETA USHINDANI MSIMU UJAO
KOCHA wa Biashara United, Amri Said amesema kuwa msimu ujao ushindani utakuwa mkali hivyo hawatafanya uzembe mwanzoni.Akizungumza na Saleh Jembe, Said amesema kuwa msimu uliopita kulikuwa na ugumu mwishoni kutokana na ushindani uliokuwepo hivyo wanatumia tahadhari hiyo kujipanga."Tulikuwa kwenye wakati mgumu kutokana na ushindani ambao ulikuwepo ila tumejifunza na tumetumia changamoto hiyo kuwa sehemu ya kufanya kitu cha kipekee,"...
NYOMI KAMA LOTE TAIFA SIMBA DAY, TIMU ZAWASILI, WALE WA BUKU TANO TIKETI ZIMEKATA
TIMU zote mbili Simba pamoja na Power Dynamo zimewasili uwanja wa Taifa kwa ajili ya kuhitimisha kilele cha SportPesa Simba Wiki. Mashabiki wengi wamejitokeza uwanja wa Taifa kushuhudia mpambano mkali ambapo tayari wengi wameingia ndani na wengine wapo nje.Wasimamizi wa Uwanja wametangaza kwamba nafasi kwa kiingilio cha shilingi 5,000 zimejaa kwa sasa.
YANGA: KIKOSI CHA KAZI HIKI LAZIMA TUTUSUE MWANZO MWISHO
MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kikosi chake kwa sasa kimetengamaa hivyo hana mashaka na ushindani wa msimu ujao pamoja na mechi za kimataifa.Akizungumza na Saleh Jembe, Zahera amesema kuwa kikubwa ambacho kinampa jeuri ya kupata matokeo chanya ni upana wa kikosi chake kwa sasa."Kikosi changu kwa sasa kina wachezaji makini ambao wanajuhudi wakiwa uwanjani, nina imani...
JUVENTUS, REAL MADRID WAPIGANA VIKUMBO KUINASA SAINI YA POGBA
REAL Madrid imeweka mezani pauni milioni 27.6 pamoja na nyota wao James Rodriguez ili kumpata kiungo wao Paul Pogba dili ambalo inaelezwa lilipigwa chini na mabosi wa United.Sasa, Juventus imeamua sasa kuweka wachezaji wake watatu ili kumpata nyota huyo kabla ya dirisha la usajili kufungwa.Ripoti zinaeleza kuwa Juventus wamemtuma kiongozi wa idara ya michezo Fabio Paratici, Makamu Mwenyekiti, Pavel...
TANZANITE KUISHUSHIA KICHAPO ZAMBIA
BAKARI Shime Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 'Tanzanite' amesema kuwa leo waapambana kupata matokeo chanya mbele ya timu ya Taifa ya Zambia.Tanzanite imefuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya COSAFA inayoendelea nchini Afrika Kusini baada ya kushinda mechi zake mbili za awali. "Tulianza kupata ushindi mbele ya Botswaa kabla ya kumalizia na...
MWENDO WA KUUJAZA UWANJA WA TAIFA KWA SIMBA UNAENDELEA
TAYARI mashabiki wa timu ya Simba wameanza kuujaza uwanja wa Taifa muda huu kuelekea mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Power Dynamo.Leo ni kilele cha SportPesa Simba Wiki ambapo ni siku rasmi kwa Simba kuwatambulisha wachezaji, jezi mpya, zitakazotumika msimu ujao pamoja na wimbo maalumu a Simba.
RATIBA YA TANZANIA KUFUZU MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA KWA MATAIFA YA AFRIKA
RATIBA ya michezo ya awali kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Burundi itakayochezwa kati ya Septemba 2-9,2019 mchezo wa kwanza ukichezwa ugenini na mchezo wa marudiano Uwanja wa Taifa.
WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MGENI RASMI LEO UWANJA WA TAIFA
SIMBA leo wanafika kilele cha SportPesa Simba Wiki ambapo uwanja wa Taifa kutachezwa mchezo wa kirafiki kati ya Simba na Power Dynamo.Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.
KMC YAONYOOSHA MABAO 2-1 KARIOBANG SHARK
KIKOSI cha KMC leo kimeibuka kidedea kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya Kariobang Sharks uliochezwa uwanja wa Uhuru.Ofisa Habari wa KMC, Anwar Bide amesema kuwa ni mwanzo mzuri kwao kuelekea mchezo wa kimataifa dhidi ya AS Kigali utakaochezwa Agosti 10."Ulikuwa ni mchezo mgumu na wenye ushindani ila mwisho wa siku tumeibuka na ushindi wa mabao...
SIMBA: TUTAKACHOFANYA SISI WAPINZANI WETU YANGA HAWAJAKIFANYA NA NI NOMA LEO
UONGOZI wa Simba umesema kuwa leo hakuna namna yoyote jambo la kwanza ni mashabiki kujaza uwanja kisha burudani zitafuata.Haji Manara Ofisa Habari wa Simba amesema:"Tunajua kwamba wenzetu wamefanya kitu kizuri ila sisi ni hatua nyingine hasa kwa ubunifu na ubora wa kile ambacho tunakifanya mwanzo mwisho. "Kila kitu kipo kwenye mpangilio bora na staili ambazo zitatumika kwenye utambulisho wa wachezaji...