AZAM FC YATOSHANA NGUVU NA RUVU SHOOTING
MCHEZO wa kirafiki uliochezwa leo kati ya Azam FC na Ruvu Shooting umekamilika kwa timu zote kutoshana nguvu.Mpaka dakika tisini zinakamilika hakuna timu iliyoona lango la mpinzani na kufanya ubao wa matokeo kusoma Azam FC 0 sawa na Ruvu Shooting.Mchezo huu umechezwa Uwanja wa Chamazi.
NAHODHA YANGA AWAITA MASHABIKI KESHO TAIFA SIKU YA MWANANCHI
PAPPY Tshishimbi, nahodha wa kikosi cha Yanga amewataka mashabiki kesho kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa kushushudia burudani.Kesho ni kilele cha siku ya Mwananchi ambapo Yanga itatambulisha wachezaji wapya pamoja na jezi mpya.Tshishimbi amesema:"Maandalizi yapo vizuri na kila kitu kipo sawa hivyo ni wakati wa mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani kuona timu yao ikipambana."Tumerejea salama na morali ni kubwa...
SPORTIPESA SIMBA WIKI YAENDELEA LEO NAMNA HII
KLABU ya Simba leo imetembelea hospital ya Ocean Road na kuwajulia hali wagonjwa pamoja na kuwapa mahitaji maalumu.Huu ni mwendelezo wa Simba kuelekea SportPesa Simba wiki inayotarajiwa kufanyika Agosti 6 uwanja wa Taifa.
DAU LA SAMATTA NOMA, GENK WAZIDI KUMKOMALIA KINOMA
UONGOZI wa klabu ya KRC Genk umeamua kuongeza tena dau kwa timu zinazomtaka mshambuliaji wake, Mtanzania Mbwana Samatta kutoka shilingi bilioni 40 hadi kufikia bilioni 53. Mshambuliaji huyo msimu uliopita alifunga mabao 23, katika Ligi Kuu ya Ubelgiji, amekuwa akitakiwa na timu nyingi za England zikiwemo Leicester, Middlesbrough na Aston Villa lakini wapo Galatasaray ya Uturuki.Taarifa za uhakika kutoka nchini...
KICHUYA: NINARUDI BONGO KUCHEZA HAKUNA TAABU
SHIZA Kichuya ameweka wazi kwamba baada ya muda wake kumalizika ndani ya klabu ya ENNPI ya Misri kwa sasa anatamani kuondoka nchini humo huku akiwa tayari kurejea Tanzania.Kichuya aliondoka Simba, Februari mwaka huu na kujiunga na ENNPI ambayo aliichezea kwa mkopo ambapo kwa sasa amerejea Tanzania mara baada ya muda wake wa mkataba kumalizika.Winga huyo amesema kwa sasa malengo...
HAJI MANARA ATANGAZA KUBWAGA MANYANGA NDANI YA SIMBA
IMEELEZWA kuwa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa anampango wa kuachia ngazi ya uongozi ndani ya Simba.Kwa sasa nafasi ya Ofisa Habari ni miongoni mwa zile ambazo zinatafuta wafanyakazi baada ya Simba kutangaza nafasi za kazi ila bado anashikilia Manara ambaye ndiye Ofisa Habari.Habari zinaeleza kuwa Manara amesema sababu kubwa itakayomfanya aachie madaraka ndani ya Simba ni...
HIZI NDIZO SABABU ZA KINDOKI KUPIGWA CHINI YANGA, MWILI JUMBA ATAJWA
MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amethibitisha kuwa ameliondoa jina la kipa wake, Klaus Kindoki katika usajili wao na kumpeleka kwa mkopo Lupopo FC ya DR Kongo.Kindoki anaondolewa Yanga kwa ajili ya kumpisha mshambuliaji mpya wa timu hiyo Mkongomani, David Molinga Ndama ‘Falcao’ ama mwili jumba akitokea Klabu ya FC Lupopo ya DR Congo kwa mkopo wa mwaka mmoja.Kipa...
YANGA WAENDELEA NA SPOTIPESA WIKI YA MWANANCHI
MASHABIKI wa Yanga wa mkaoni Njombe wamendelea na wiki ya SportiPesaWikiYaMwanachi kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii.Licha ya baridi kali ya mkoani Njombe, haikuweza kuwazuia Wanayanga kwa kuwatembelea watoto wenye uhitaji na kufanya shughuli mbalimbali za kijamii.Wiki ya Mwananchi kilele chake ni kesho uwanja wa Taifa ambapo mbali na kucheza na Kariobangi Sharks watatambulisha jezi mpya na wachezaji.
KIKOSI CHA MAUAJI CHA MBAO FC MSIMU WA 2019/20
KIKOSI kazi cha Mbao FC msimu wa 2019/20 kipo namna hii:-
KUMUONA SIBOMANA, JUMA BALINYA NI BUKU TANO TU TAIFA
UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kuelekea siku ya kilele cha Mwananchi Agosti 4 mambo yamekamilika kwa asilimia kubwa ni suala la mashabiki kujitokeza kwa wingi.Kesho Jumapili uwanja wa Taifa kutakuwa na shughuli maalumu kwa Yanga kutambulisha wachezaji wapya wa tiu kwa ajili ya msimu mpya wa 2019/20 pamoja na kuzindua wimbo mpya wa Yanga.Pia uzi mpya wa Yanga utazinduliwa...