SENEGAL WAPATA PIGO LEO KUMKOSA BEKI WAO KISIKI FAINALI YA AFCON
KALIDOU Koulibary beki mahiri wa timu ya Taifa ya Senegal leo ataukosa mchezo wa fainali kwenye michuano ya Afcon dhidi ya Algeria nchini Misri.Hii inatokana na beki huyo kisiki kuwa na kadi mbili za njano.Inakuwa ni mara ya kwanza kwa Senegal kumkosa nyota wao anayekipiga kwenye timu ya Napol ya Italia.Hili ni pigo kwa Senegal kwani ni miongoni mwa...
SIMBA KUCHEZA KWENYE MIJI MITATU SAUZI
SIMBA ambayo ipo kambini nchini afrika Kusini ambapo inatajwa kambi hiyo ni ghrama kubwa, imetangaza kuwa itacheza michezo mitatu ya kujipima nguvu. Kumekuwa na maswali mengi kuhusiana na kambi ya Simba huko Afrika Kusini, huku Watanzania wanaoishi nchini humo wakihoji timu hiyo imepata wapi fedha za kukaa kwenye kambi ya kisasa namna hiyo.Simba wameweka kambi sehemu moja na mabingwa...
USAJILI YANGA WAZUA HOFU SIMBA
WAKATI kikosi cha Yanga kikiendelea kujifua huko mkoani Morogoro kwa ajili ya msimu ujao wa ligi, aliyekuwa kipa namba moja wa timu hiyo, Beno Kakolanya ametishwa na usajili uliofanywa na klabu hiyo.Kakolanya ambaye sasa yupo Afrika Kusini na kikosi cha Simba baada ya kusajiliwa hivi karibuni, alisema kutokana na usajili huo ambao Yanga imeufanya hivi karibuni, anaamini msimu ujao...
KOCHA SIMBA AIBUKA NA LAKE BAADA YA KASEJA KUITWA STARS
Mchezaji wa zamani wa Simba Abdallah King Kibadeni, amesema kitendo cha Kocha Etienne Ndairagije kumuita Kipa Juma Kaseja kunako kikosi cha Taifa Stars ni maamuzi mazuri.Kibadeni ameeleza kuwa kuitwa kwa Kaseja kutatoa nafasi kwa magolikipa wanaochipukia kujifunza mambo mengi kutoka kwake.Kibadeni amesema bado Kaseja ana mchango mkubwa wakuendelea kuwepo kwenye kikosi cha Stars kutokana na uzoefu aliokuwa nao, akisema...
CAF YAIFANYIA MABADILIKO TAIFA STARS
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) katika kikao chake kilichokaa Julai 17,2019 kimefanya marekebisho ya michezo ya kufuzu Fainali za Afrika (AFCON) 2021.Hatua ya awali kufuzu itachezwa kati ya Oktoba 7-15,2019 wakati michezo mingine itakua kati ya Novemba 11-19,2019.Michezo inayofuata itachezwa kati ya Agosti 31, 2020 na Septemba 8, 2020 na hatua inayofuata kuchezwa...
KASEJA, YONDANI KUIONGOZA KAMBI STARS – VIDEO
Kipa Mkongwe wa Tanzania na klabu mbalimbali vya Ligi kuu Tanzania Bara Juma Kaseja ameitwa katika kikosi cha timu ya Taifa kwa mara ya pili tokea kipindi cha aliyewhi kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa, Maxmo.Hii inakuja baada ya kocha Etiene Dailangije kuchukua mikoba ya ya Emmanuel Amunike ambaye alikuwa akikinoa kikosi hicho, ambaye hata hivo anakinoa kikosi...
WALIOKATAA FEDHA ZA UWOYA GLOBAL WAPEWA KITITA
UONGOZI wa Global Publishers umewapongeza kwa kuwapa kitita cha fedha wanahabari wake, Imelda Mtema na Hillary Daudi, kwa kuonesha weledi wa kutogombea fedha wakati mwigizaji wa Bongo Movies, Irene Uwoya alipowamwagia fedha waandishi wa habari waliojitokeza katika Ukumbi wa Hyatt Kilimanjaro jijini Dar, hivi karibuni kwenye mkutano ulioitishwa na wasanii wa tasnia ya filamu nchini.Tukio hilo la Uwoya lilielezwa...
HILI NDILO KUNDI LA TANZANIA KUFUZU AFCON CAMEROON 2021
Timu ya Taifa ya Tanzania imeanzia hatua ya makundi ya kuwania kufuzu Fainali ya Mataifa ya Afrika mwaka 2021 itakayofanyika nchini Cameroon.Tanzania imepangwa kundi J ikiwa na timu zifuatavyo Tunisia, Libya na Equatorial Guinea.
NYOTA WANNE WA SIMBA WATUA AFRIKA KUSINI, WAANZA KAZI RASMI
TAYARI nyota wanne wa Simba ambao walikuwa wamekwama kukwea pipa na kujiunga na timu nchini Afrika Kusini wameshatia timu na leo wamefanya mazoezi na wachezaji wengine.Wachezaji hao ambao ni Meddie Kagere, Deo Kanda, Francis Kahata na Sharaf Shiboub walikwama kuondoka na timu Jumatatu kutokana na kushughulikia paspoti.Simba imeweka kambi ya muda wa wiki mbili nchini Afrika Kusini kwa ajili...