Home Uncategorized AZAM FC YAWAITA MASHABIKI KUIPASAPOTI KIMATAIFA

AZAM FC YAWAITA MASHABIKI KUIPASAPOTI KIMATAIFA

BAADA ya Caf kutoa ratiba ya awali ya michuano ya Afrika, uongozi wa Azam FC umewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuwapa sapoti.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa klabu inatoa fursa kwa mashabiki kujiunga nao kuelekea nchini Ethiopia.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi na tumeweka utaratibu wa kuwapokea mashabiki wetu, na kuna mpango wa kukata tiketi pamoja na viza hivyo ni vitu muhimu ambavyo wanatakiwa kuwa navyo, wakijitokeza kwa wingi tutatoa ushirikiano,” amesema.

Mchezo wa kwanza utachezwa nchini Ethiopia kati ya Agosti 9-11 na ule wa marudio utachezwa kati ya Agosti 23-25 utachezwa Dar.

SOMA NA HII  TAIFA STARS KAMILI KUIVAA BURUNDI, KUINGIA KAMBINI LEO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here