Home Uncategorized KIUNGO SIMBA AMWAGIA SIFA USAJILI WA SHIKALO YANGA

KIUNGO SIMBA AMWAGIA SIFA USAJILI WA SHIKALO YANGA


Kiungo wa zamani wa Simba Mkenya, Jerry Santo ameonyesha hisia zake kwa Yanga juu ya usajili wa kipa, Farouk Shikalo.

Kwa mujibu wa gazeti la Spoti Xtra, Santo alisema kuwa Yanga imepata bonge la kipa ambaye kamwe wapenzi na mashabiki wa timu hiyo hawatajutia mamilioni yao ya fedha waliyoyatoa kumsajili kipa huyo.

Alisema mapungufu yote ambayo msimu uliopita yalijitokeza katika eneo la kipa baada ya kuondoka kwa Beno Kakolanya, sasa wameyapatia ufumbuzi na anawapongeza kwa kufanikisha usajili huo.

“Yanga wamepata bonge la kipa, Shikalo ni kipa bora kabisa hapa Kenya kwani amekuwa akifanya vizuri sana na ninaamini atakuwa msaada mkubwa kwa ndugu zangu hao wa Yanga.

“Mimi bado nacheza soka hapa Kenya nipo katika timu ya ligi kuu ya Posta
japokuwa mara nyingi nimekuwa nikitumika kama kocha mchezaji hivyo Shikalo namjua vizuri sana, kwa hiyo basi Yanga wamepata kipa mzuri, wapinzani wajipange tu kuiona kazi yake uwanjani,” alisema Santo.

SOMA NA HII  MAAMUZI MAGUMU KUFANYIKA NDANI YA SIMBA, MBADALA WA SVEN ATAJWA