Home Uncategorized KOCHA YANGA ATAKA VIONGOZI WAJIEPUSHE NA SUALA LA USAJILI

KOCHA YANGA ATAKA VIONGOZI WAJIEPUSHE NA SUALA LA USAJILI


KOCHA wa timu ya Vijana wa Yanga, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’, amesema kuwa ni wakati sahihi kwa viongozi kuwaachia majukumu makocha masuala ya usajili ili kuepusha migogoro.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mmachinga amesema kuwa kumekuwa na tabia ya viongozi kupendekeza majina ya wachezaji wanaowataka jambo ambalo litaigharimu timu.

“Kuna baadhi ya viongozi wana tabia ya kupendekeza majina ya wachezaji na kukamilisha usajili, hili ni gumu na linachangia migogoro ndani ya timu.

“Ni busara viongozi kufanyia kazi ripoti ya mwalimu ili kupata wachezaji ambao wanastahili na kumuachia maamuzi mwalimu,” amesema.

SOMA NA HII  ALIYEFANIKISHA DILI LA SAMATTA KUKIPIGA ASTON VILLA APIGWA CHINI MAZIMA