Home Uncategorized TANZANIA KESHO KAZINI KUMENYANA NA UGANDA MICHUANO YA CECAFA

TANZANIA KESHO KAZINI KUMENYANA NA UGANDA MICHUANO YA CECAFA


KIKOSI cha Timu ya Taifa la Tanzania chini ya miaka 15 Kwa sasa kipo nchini Eritrea kwa ajili ya kushiriki michuano Kwa CECAFA kwa timu za Vijana walio chini ya miaka 15.

Tanzania imepangwa kundi B lenye timu tano ambazo ni Rwanda, Uganda, Sudani ya Kusini na Ethiopia.

Kesho, Agosti 19 itashuka Uwanja wa Asmara kumenyana na timu ya Uganda mchezo wake wa Kwanza.

Kocha wa Tanzania, Maalim Saleh ‘Romario’ amesema maandalizi yapo sawa na imani ni kubwa kwa timu kupata matokeo. 

“Tupo vizuri na tunatambua kuwa mashabiki wanapenda kuona tunapata ushindi, rai yangu kwao wasisahau kutuombea na kutupa sapoti,” amesema.
SOMA NA HII  KOCHA MKUU WA SIMBA ATAJA KITAKACHOMREJESHA MLIPILI KIKOSI CHA KWANZA