Home Uncategorized WAPINZANI WA YANGA KIMATAIFA WANYAKA MAFAILI YANGA WANA KAZI YA ZIADA KESHO

WAPINZANI WA YANGA KIMATAIFA WANYAKA MAFAILI YANGA WANA KAZI YA ZIADA KESHO


WAPINZANI wa Yanga kimataifa timu ya Township Rollers wameanza kuwasomea ramani wapinzani wao Yanga kabla ya kesho kwa kuiba mbinu zao kabla ya kukutana nao uwanja wa Taifa.

Yanga itawakaribisha kesho Township Rollers kutoka Botswana kwenye mchezo wa kwanza wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa uwanja wa Taifa.

Leo Township Rollers wamekaa na kuangalia baadhi ya mechi za Yanga ikiwa ni sehemu ya kuangalia aina ya uchezaji wao kupitia baadhi ya video.

Inaelezwa kuwa Rollers sio watu wazuri wakiwa uwanjani kwani wana spidi ya hatari na uwezo wa kufunga kwa kushtukiza hivyo Yanga wana kazi ya ziada kuzuia mashambulizi ya wapinzani wao.

Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema wana kazi kubwa ya kufanya ila imani yao ni kupata matokeo chanya. 

SOMA NA HII  KISA SAMATTA, SERIKALI YATOA AGIZO KWA WACHEZAJI