Home Uncategorized DIJK ILIBAKI KIDOGO ATUE MANCHESTER UNITED, ALIYEZUIA DILI LAKE HUYU HAPA

DIJK ILIBAKI KIDOGO ATUE MANCHESTER UNITED, ALIYEZUIA DILI LAKE HUYU HAPA


JOSE Mourinho aliyekuwa meneja wa Manchester United inaelezwa kuwa alimchunia jumla beki wa Liverpool, Virgil Van Dijk.

United ilikuwa kwenye harakati za kuinasa saini ya beki huyo ambaye ana tuzo ya Beki Bora wa Ulaya kwa sasa pia anawania Tuzo ya Ballon d’Or akiwa ametimiza jukumu la kuipa timu yake taji la ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita.

Taarifa zinadai kuwa Mourinho aliwaambia mabosi wake kuwa hesabu zake kubwa ni kwa Eric Bailly na Victor Lindelof ambao alikuwa anawaamini. 

Baada ya msimu mmoja kumkataa beki huyo raia wa Uholanzi Mourinho alifukuzwa kazi msimu wa mwaka 2018 kutokana na matokeo mabovu na hatimaye United imetoa paauni milioni 85 kumpata beki wa kati Harry Maguire kiwango ambacho ni kikubwa kinoma.

SOMA NA HII  YAKUB NA ABAROLA MAMBO BADO MAZITO GHANA