Home Uncategorized MWANARIADHA AJUNGA NA KLABU YA SOKA

MWANARIADHA AJUNGA NA KLABU YA SOKA


Bingwa mara mbili wa mbio za mita 800 kwenye michezo ya Olimpiki, Caster Semenya (28) ameanza kujiandaa kwa maisha mapya nje ya riadha baada ya kujiunga na klabu moja ya soka ya wanawake

Mwanariadha huyo kwa sasa anakata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama ya Kusikiliza kesi za michezo (CAS) iliyoidhinisha matumizi ya sheria za Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF) zinazotaka wanawake walio na homoni za juu za ‘testosterone’ kutumia dawa kuzipunguza kabla ya kushiriki mashindano yoyote kitu ambacho amekataa kufanya

Raia huyo wa Afrika Kusini ameanza kufanya mazoezi na klabu ya JVW FC kutoka mjini Gauteng akinuia kusakata mechi yake ya kwanza msimu ujao kwa sababu wakati huu kipindi cha kusajili wachezaji kimefungwa.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI