Home Uncategorized WACHEZAJI STARS WAFANYA MGOMO

WACHEZAJI STARS WAFANYA MGOMO


Wakati wa mapumziko wachezaji wa kikosi cha Taifa Stars juzi waligoma kuingia vyumbani ili kuwavuruga kisaikolojia wenyeji katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia Qatar 2022 dhidi ya Burundi.

Stars waligoma kuingia vyumbani baada ya kuhisi harufu za ajabu ambazo walikuwa hawazielewi, hivyo viongozi wakashauri wabaki nje.

Katika mzozo huo, Watanzania watatu, walikamatwa na wanajeshi wa Burundi na kuwekwa kizuizini hadi tunakwenda mitamboni walikuwa hawajaachiwa.

Kikosi cha Stars: Juma Kaseja, Haruna Shamte, Gadiel Michael, Kelvin Yondani, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Sure Boy, Himid Mao, Samatta, Msuva na Hassan Dilunga.

SOMA NA HII  FA FAINALI: SIMBA 2-0 NAMUNGO FC