Home Uncategorized KASI YA NYOTA MPYA WA SIMBA YAMKOSHA MBELGIJI WA SIMBA, ALICHOKIFANYA DAKIKA...

KASI YA NYOTA MPYA WA SIMBA YAMKOSHA MBELGIJI WA SIMBA, ALICHOKIFANYA DAKIKA 12 NI BALAA


DAKIKA 12 za kiungo mpya wa Simba, Luis Miqoissone  akitokea benchi kuchukua nafasi ya Hassan Dilunga  zimemkosha Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vanderbroeck ambaye alibaki akitikisa kichwa kuonyesha kwamba amekubali uwezo wa nyota huyo.
 Raia huyo wa Msumbiji aliyetokea timu ya UD Songo na kusaini kandarasi ya miaka miwili alikuwa na kasi ya kuitafuta mipira na kutoa pasi kwa wachezaji wenzake kwa umakini.
Jezi yake mgongoni ni namba 11 iliwahi kuvaliwa na  mshambuliaji wa zamani Laudit Mavugo na ilikuwa ikivaliwa na mbrazil, Wilker da Silva ndani ya dakika 12 alizotumia kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi uwanja wa Gombani dhidi ya Zimamoto alisababisha faulo mbili kutokana na kuchezewa rafu na wachezaji wa Zimamoto .
Habari kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa bado Sven anamvutia kasi nyota huyo ili kuona ni namna gani ataweza kuingia kwenye mfumo wake mpya wa kikosi chake cha kwanza.
Ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Zimamoto umeipa nafasi Simba kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi na leo itamenyana na Azam FC kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali.

Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola amesema kuwa ni ngumu kuzungumzia mchezaji huyo kwenye mechi ya kwanza kwani bado mechi zipo.
SOMA NA HII  NAMNA TAMBWE ANAVYOTUONYESHA MAKOSA YA USAJILI KATIKA KLABU ZETU