Home Uncategorized BIRTHDAY YA YANGA ILIVYOTIBULIWA

BIRTHDAY YA YANGA ILIVYOTIBULIWA


Bernad Morrison, mshambuliaji wa Yanga, juzi ameonyesha ushujaa wake mbele ya Mbeya City kwa kufunga bao la kiufundi kwenye sare ya bao 1-1 mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Siku hiyo ilikuwa siku muhimu kwa Yanga ambao wametimiza miaka 85 kuanzia timu hiyo ilipoanzishwa mwaka 1935.

Hata hivyo, keki iliyokuwa imeandaliwa haikuliwa kwa furaha baada ya sare hiyo ambayo inawafanya waendelee kuwaza mara mbili kama kweli wanaweza kubeba ubingwa msimu huu.

Yanga ambao walionekana kuwa na morali ya hali ya juu uwanjani jana walikosa matokeo tu, lakini walionyesha kandanda safi  sana huku wakipoteza nafasi kadhaa za wazi.

Mbeya City ambao kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza walitoka suluhu na Yanga kwenye Uwanja wa Sokoine, walianza kupata bao la kuongoza dakika ya 42 baada ya beki wa Yanga, LamineMoro kujifunga wakati akihaha kuokoa.

Kipindi cha pili Yanga wakiongeza mashambulizi kupitia kwa Ditram Nchimbi aliyekuwa akipiga krosi kichwa akipata krosi kutoka kwa beki mahiri kwa sasa Juma Abdul.

Hili ni bao la pili kwa Morrison ndani ya ligi na kuwafanya Yanga wagawane pointi moja na Mbeya City iliyo chini ya beki wa zamani wa Simba, Amri Said.

Kwenye mechi nyingine ya Ligi Kuu Kati ya Ruvu Shooting na Tanzania Prisons, iliyotakiwa ichezwa Uwanja wa Mabatini imeahirishwa ukisubiri maamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na Ruvu Shooting kushindwa kuwahisha Ambulace ambayo ilichelewa kufi ka uwanjani kwa zaidi ya dakika 35.
SOMA NA HII  WATU WAENDELEA KUCHOTA MKWANJA NDANI YA SPORTPEA, CHALII AONDOKA NA MILIONI 6 NA USHEE