Home Uncategorized JEMBE LA MTIBWA SUGAR LIMERUDI, RASMI KUANZA KAZI KESHO

JEMBE LA MTIBWA SUGAR LIMERUDI, RASMI KUANZA KAZI KESHO

UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa nyota wao Salum Kihimbwa amerejea rasmi uwanjani kutokana na kupona majeraha yake.

Kihimbwa alikuwa nje ya kikosi hicho cha Mtibwa kilicho chini ya Zuber Katwila tangu Februari 2.

Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa wana imani anaweza kucheza mchezo wa kesho dhidi ya Ndanda FC.

Kwenye mechi saba ambazo Mtibwa Sugar wamecheza mwezi Februari imekuwa ngumu kufurukuta kwa kupata matokeo kwani wamepoteza mechi sita na kuambulia pointi moja.

SOMA NA HII  SIMBA YACHANGIA YANGA KUPOTEZA MBELE YA KMC NAMNA HII