Home Uncategorized KLOPP APASUA KICHWA KUMKOSA WIKI TATU NYOTA WAKE HENDERSON

KLOPP APASUA KICHWA KUMKOSA WIKI TATU NYOTA WAKE HENDERSON


JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa kiungo wake Jordan Henderson atakuwa nje kwa muda wa wiki tatu kutokana na majeraha aliyopata.

Nyota huyo anasumbuliwa na majeraha ya nyama za paja na kuna hofu kuwa hataweza kucheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid.

Kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Hispania Liverpool ilinyooshwa kwa kufungwa bao 1-0 mechi ya pili inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa itamtoa mshindi atakayetinga hatua ya robo fainali.

“Nafikiri inaweza kuwa kati ya wiki tatu ama zaidi ya hapo kutokana na majeraha aliyonayo na yanaonekana kuwa mabaya sana kwetu,” amesema.

SOMA NA HII  NONGA: MUHIMU KWA WACHEZAJI KUCHUKUA TAHADHARI NA KUFANYA MAZOEZI