Home Uncategorized BERNARD MORRISON ASHANGAZWA NA MASHABIKI WA YANGA

BERNARD MORRISON ASHANGAZWA NA MASHABIKI WA YANGA

BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa mchezo wake wa kwanza dhidi ya Singida United alishangazwa na mashabiki wake kwa kumpa zawadi ya fedha jambo ambalo hakuritarajia.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Namfua, Morrison alitoa pasi yake ya kwanza ya bao lililofungwa na kiungo mwenzake, Haruna Niyonzima.

Morrison amesema :’Baada ya mchezo wetu dhidi ya Singida United mashabiki waliniita nikadhani kwamba wanahitaji tupige nao picha lakini ghafla kila mmoja akatoa fedha mmoja elfu kumi mwingine elfu tano jambo ambalo nilikuwa sijalizoea awali na ninafurahishwa na upendo wa mashabiki,” .

Kwenye mchezo wake wa kwanza wa dabi dhidi ya Simba, Morrison alifunga bao la ushindi dakika ya 44 kwa njia ya faulo na kuipa pointi tatu timu yake.

SOMA NA HII  MUANGOLA WA YANGA ALIGOMA KWENDA KUCHEZA ULAYA, KISA YANGA