Home Uncategorized KOCHA LIVERPOOL AMKINGIA KIFUA MLINDA MLANGO WAKE, ATAJA SABABU ZA KICHAPO

KOCHA LIVERPOOL AMKINGIA KIFUA MLINDA MLANGO WAKE, ATAJA SABABU ZA KICHAPO


JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa kichapo walichokipata mbele ya Atletico Madrid kwa kufungwa mabao 3-2 ni uzembe wao wenyewe wa kuchelewa kufunga bao ndani ya dakika tisini za mwanzo na sio kosa la mlinda mlango wao Adrian.
Liverpool imetolewa kwenye mbio za kuwania Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 na kuwaacha wapinzani wao Atletico Madrid wakitinga hatua ya robo fainali baada ya kupata ushindi wao wa pili wakiwa ugenini kwani kwenye mchezo wa kwanza Atletico walishinda bao 1-0 na kuwafanya wapenye kwa jumla ya mabao 4-2.
Liverpool ilipata bao la kwannza dk dk ya 43 kupitia kwa Georginio Wijnaldum lilidumu dakika 90 zilizopelekea kuongezwa dakia 30 ili kumpata mshindi  ambapo waliongeza bao la pili dk ya 94 kupitia kwa Roberto Firmino lilidumu kwa muda wa dakika tatu ambapo Atletico Madrid walifunga kupitia kwa Marcos Liorente dk 97 ambaye alikomelea msumari wa mwisho dk ya 105+1.

Bao la pili kwa Atletico Madrid lilifungwa na Alvaro Morata liliifanya Liverpool kupoteza matumaini ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa na kulipoteza Kombe lao lililokuwa mikonini mwao.


Klopp amesema kuwa anakubali uwezo wa mlinda mlango wake kwani hakuwa na chaguo la kufanya kutokana na wachezaji kushindwa kupata mabao mengi ndani ya dakika 90 za mwanzo na amewapongeza wapinzani wake kwa kucheza mchezo mzuri.

Adrian ni mlinda mlango namba mbili alipata nafasi ya kudaka baada ya mlinda mlango namba moja wa kikosi hicho Allison Becker kuwa majeruhi, alitoa pasi ambayo ilimkuta mchezaji wa Atletico Madrid Marcos ambaye alimtungua akiwa langoni mwake.
SOMA NA HII  STAILI MPYA SIMBA YA KUKABA SI MCHEZO