Home Uncategorized KOSAKOSA ZA KAGERE KWA YANGA BADO ZIPO KICHWANI MWAKE, HIKI HAPA AMESEMA

KOSAKOSA ZA KAGERE KWA YANGA BADO ZIPO KICHWANI MWAKE, HIKI HAPA AMESEMA


MEDDIE Kagere, mshambuliaji wa Simba amesema kuwa nafasi mbili alizomkosa mlinda mlango wa Yanga, Metacha Mnata kwenye dabi ya Kariakoo huwa zinamkosesha raha.

Kagere alikosa nafasi mbili za kufunga kwenye mchezo huo uliochezwa Machi 8 Uwanja wa Taifa na Simba ikafungwa kwa bao 1-0.

Moja Kati nafasi hizo Kagere aliachia shuti kali nje ya 18 kwa guu la kushoto ikagonga mwamba na kurudi uwanjani na nafasi nyingine aliyoipata Mnata aliinyaka.

Kagere amesema katika dabi hiyo bahati haikuwa yao kwani walipata nafasi nyingi za kufunga wakazidiwa na wapinzani wao. 


“Nafahamu mashabiki wa Simba wameumia baada ya matokeo ya kufungwa na Yanga, maumivu hayo wanayoyapata sisi pia tunayapata . 

“Tulipanga kushinda katika mchezo ule lakini bahati haikuwa nzuri kwetu mapungufu yetu Kocha ameyaona atayafanyia kazi, zile nafasi huwa zinaniuma”.

Kagere ni kinara wa utupiaji akiwa na mabao 19 ndani ya Ligi Kuu Bara, msimu uliopita 2018/19 alitupia mabao 23.

SOMA NA HII  ACHENI KULALAMIKA, UNACHOPATA SASA NI KILE ULICHOPANDA 2018/19