Home Uncategorized MEDDIE KAGERE WA SIMBA ATAJA SABABU YA KUCHEKA NA NYAVU

MEDDIE KAGERE WA SIMBA ATAJA SABABU YA KUCHEKA NA NYAVU


MEDDIE Kagere, mshambuliaji wa Simba amesema kuwa kikubwa kinachompa mafanikio ni ushirikiano anaoupata kutoka kwa wachezaji wenzake na kutimiza majukumu yake ndani ya kikosi hicho.

Kagere ni kinara wa utupiaji akiwa na mabao 19 na alifunga hat trick yake ya kwanza msimu huu wa 2019/20 mbele ya Singida United kwenye ushindi wa mabao 8-0 mchezo uliochezwa Uwanja wa uhuru.

Kagere amesema:”Kikubwa ni ushirikiano na sapoti kutoka kwa wachezaji wenzangu pamoja na mashabiki, ninaamini kuna mengi ambayo yanakuja kutokana na ushirikiano huu, ninawaomba mashabiki waendelee kutupa sapoti,” amesema.

Simba imefunga mabao 63 ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo na pointi zake ni 71.

SOMA NA HII  NDEMLA: NITASAINI YANGA