Home Uncategorized VITA YA KUWANIA SAINI YA NYOTA WA SIMBA NA TP MAZEMBE NI...

VITA YA KUWANIA SAINI YA NYOTA WA SIMBA NA TP MAZEMBE NI BALAA


VITA ni kali kati ya Klabu za Simba na TP MAzembe ya DR Congo ambapo kila moja inataka kumchukua mshambuliaji Deo Kanda. 

Nyota huyo anayecheza Simba kwa mkopo akitokea katika timu ya TP Mazembe ya Congo, msimu huu kwenye ligi kuu amefanikiwa kuwafungia mabao saba hali inayoonyesha kuwa Msimbazi wamenogewa naye.

Chanzo kutoka ndani ya Simba kimeliambia Championi Jumamosi kuwa, Simba inataka kumpa nyota huyo mkataba wa kudumu huku uongozi wa TP Mazembe nao ukiwa katika hatua za kutaka kumrejesha staa huyo kikosini mwao.
“Sisi kwa upande wetu hatuna neno na Kanda na tutakuwa wajinga leo hii tukisema kuwa ni mchezaji mbaya kwani tumeona uwezo wake ulivyo mkubwa na tumeona kuwa atatusaidia na ndiyo maana tunahitaji kumpa mkataba wa kudumu.
“Lakini shida inaweza ikawa kwa upande wa uongozi wa TP Mazembe kwani wanataka kumrudisha katika kikosi chao na unajua Kanda alikuwa hachezi kwa kuwa walikuwa na maelewano mabovu na kocha Mihayo Kazembe ambaye kuna taarifa anaweza akaondolewa katika timu hiyo,” kilieleza chanzo hicho.
SOMA NA HII  UNAAMBIWA GSM BABA LAOO..WARUDI YANGA KWA SPIDI 360..!!