Home Uncategorized ANAYEWINDWA NA YANGA AANZA KUAGA RASMI KWA MABOSI WAKE

ANAYEWINDWA NA YANGA AANZA KUAGA RASMI KWA MABOSI WAKE


PAUL Nonga, nahodha wa Lipuli ambaye saini yake inaelezwa inawindwa na mabosi wake wa zamani Yanga amewaaga mabosi wake wa Lipuli rasmi ili asepe msimu ujao.

Nonga amekuwa kwenye ubora wake msimu huu ndani ya Lipuli akiwa amefunga mabao 11 na kutoa pasi nne za mabao kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.

Mkataba wake ndani ya Lipuli umebakisha miezi sita ambapo tayari mabosi hao walianza kufanya naye mazungumzo ili kupata saini yake msimu ujao.

“Nimewaambia viongozi wa Lipuli kwamba kwa sasa ninahitaji kupata changamoto mpya ili waaanze kutafuta mbadala wangu mapema kwani msimu ujao ninaondoka,” amesema Nonga.

Chanzo: Championi

SOMA NA HII  SABABU ZA JKT KUSHINDWA KUTAMBA ZAWEKWA WAZI