Home Uncategorized FUNGIAFUNGIA IMEANZA NI MUHIMU KWA WENGINE KUONGEZA UMAKINI

FUNGIAFUNGIA IMEANZA NI MUHIMU KWA WENGINE KUONGEZA UMAKINI


Waswahili wanasema mwenzio akinyolewa basi ujiandae kwa kutia maji kichwani yaani uwe tayari kwa kunyolewa na wewe.
Unajua nimesema hivyo kwa nini? Kwasababu fungia fungia ya viwanja kucheza bila mashabiki imeanza.
Imeanzia Dodoma kwa JKT Tanzania kwa uwanja wao wa Jamhuri kufungiwa na sasa watacheza bila mashabiki na wengine wajiandae pingu iko njiani inakuja.
Uwanja wowote ule wa nje ya Dar es Salaam ambako hizi timu kongwe za Simba na Yanga zitaenda kucheza kwa wakati huu basi niseme wajiandae kwa hilo.
Sina hakika kama wataweza kuwadhibiti mashabiki watakaomiminika kwenye viwanja vyao kwasababu hizo timu zitavuta kijiji au mitaa wanatembea navyo kila wanakokwenda.
Kingine viwanja vyetu vina mfumo wa kizamani na miundombinu yake ni ya kizamani pia hivyo tusidanganyane kama kuna watu wataweza kudhibiti mashabiki wasijazane kwenye viwanja vyao.

Suala jingine gumu ndio litakalo watesa wengi ni fedha na hilo ndio gumu zaidi au tuseme ndio mchawi mwenyewe.
Ujio wa Simba na Yanga kwenye uwanja wako  basi ni wakati wa kuvuna hilo halina ubishi hata kidogo na viongozi wote wa viwanja vya nje ya Dar es Salaam wanafahamu hilo.
Huo ni muda wa mavuno kwao yaani neema inakuwa imedondoka maana michezo mingine mingi haina uwezo wa kuvuta mashabiki wengi kama Simba na Yanga.
Na ndio maana timu nyingi hasa zile ambazo Simba na Yanga hazijaenda kwenye viwanja vyao ziliongoza kwa kupambana kukataa ule mfumo wa kwanza uliotolewa na Serikali wa kucheza kwenye kituo kimoja.
Walikataa kwa sababu walijua fika watakosa mavuno wakati miamba hiyo ikitua kwenye mikoa yao.
Sasa niwaambie tu mjiandae pingu ya kufunga viwanja inakuja imeanzia Dodoma inatembea kila mkoa ambao hivyo vigogo vitapita.
SOMA NA HII  KAMA ULIVYOSIKIA SIMBA WAKUBALI KIPIGO DADIKA ZA LALASALAMA