Home Uncategorized MWAMNYETO AMUIBUKIA KAGERE

MWAMNYETO AMUIBUKIA KAGERE

BEKI wa Coastal Union, Bakari Mwamnyeto ‘Nondo’ ameonyesha kuukubali muziki wa straika wa Simba, Meddie Kagere, huku akisisitiza ni moja ya wachezaji wanaomfanya kujituma zaidi.

Kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii, straika wa Simba, Kagere, aliposti ujumbe kwamba ni vyema kuzungumza kwa maneno kuliko kukaa kimya jambo lililomuibua beki huyo na kumpongeza straika huyo Mnyarwanda. 

Akizungumza na Gazeti la DIMBA Jumatano, Mwamnyeto alisema, mara zote amekua muumini mzuri wa wachezaji wenye uwezo zaidi yake huku akiamini wamekuwa wakimpa chachu wanapocheza mechi pamoja.

Alisema Kagere ni moja ya mastraika bora wa mfano ndani ya soka la Tanzania, hivyo wakati wote amekuwa akimfuatilia na kujifunza mambo mengi kutoka kwake.

“Si Kagere tu, wapo wachezaji wenye uwezo mzuri ambao wakati mwingi nawafuatilia, najifunza vingi kutoka kwao na pia wanazidi kunipa shauku ya kupambana zaidi uwanjani,” alisema Mwamnyeto.

Beki huyo ambaye pia anakitumikia kikosi cha timu ya taifa, anatajwa kuwa moja ya wachezaji wanaowaniwa na vigogo wa soka Simba na Yanga na asilimia kubwa huenda akatua Jangwani msimu ujao. 

SOMA NA HII  ALIYEMCHEZEA RAFU FEI TOTO ARUDI KWA MASHABIKI KUOMBA MSAMAHA